Cheo Ni Dhamana: Jamii Hulipa Fadhira

By admin Nov 12, 2024

CHEO NI DHAMANA YA KIJAMII, UKIKIPATA IJALI JAMII YAKO, KIKIFIKA MWISHO RUDI KWENYE JAMII: JAMII INA KAWAIDA YA KULIPA FADHIRA

_Uchambuzi wa Kijamii na Kisiasa (kuelekea chaguzi za 2024/2025)_

Na:-

Titho Philemon

Wanazuoni wawili wa Kihindi wajulikanao kama *Sunil Luthra*, *Ravinder K. Kharb* wakiwa katika utafiti wao wa kuona ni namna gani uwekezaji wao wa kimkakati ungeweza kuwalipa, *walifanikiwa* kuibuka na kanuni moja ijulikanayo kama “Payback Period”. 

Kwa mujibu wa wanazuoni hao, kusudi kuu la kuhesabu kipindi cha malipo (payback period) ni kuamua wakati ambapo mtaji uliowekezwa katika mradi utarejeshwa kwa faida na kumnufaisha mwekezaji.

BINAFSI, *Mimi kama sehemu ya wananchi wa NGARA na Tanzania* kwa ujumla kuelekea chaguzi za 2024/2025 NINATEGEMEA KUONA jamii ikiwalipa wanasiasa na wanaotaka nyadhifa za uongozi sawa sawa na uwekezaji wao katika jamii hizo (wanazogombea uongozi). Wanangara tunatambua kuwa historia, vyeo vya mgombea, elimu yake pamoja na uchumi wake pia *havitoshi kututia moyo WanaNgara* kama mgombea huyo hakuwahi kushikamana nasi kama jamii katika kipindi ambacho mgombea huyo alikuwa katika nafasi nzuri ya kutusaidia. 

Wanajamii wa Ngara *ni haki yetu na TUKO TAYARI kulipa fadhira (Paybacks)* kwa kiongozi ambaye ataonekana kuwa chaguo la Wananchi na ambaye ataaminiwa na kupewa baraka za wananchi kwa kadri ya upendo ambao atakuwa amewahi kuwaonyesha.

Unataka Uenyekiti wa Mtaa, Udiwani au Ubunge ndiyo, lakini Je jamii inaimani na wewe katika kiasi ambacho kitawafanya wakupe kura za kutosha pamoja na ushirikiano kama sehemu ya fadhira ya kujaminiana kwako?

TUKIWA TUNAENDELEA KUSUBIRIA HUKUMU YA KWELI YA WANAJAMII KWENYE MABOKSI YA KURA 2024/2025 :-

*1. Tuendelee kuuishi uhalsia wetu (Let us Be Real)*

Hakuna haja ya kujihudhurisha kwenye misiba, sherehe na Tafrija mbalimbali za kijamii kama haikuwa Desturi yako. Kubembeleza kura hakujawahi kumuacha mtu salama. Subiria Muda sahihi Jamii ina kawaida ya kulipa fadhira!

2. Tuzidi kunadi sera zaidi kuliko kutungiana vijembe na Kashfa

Jamii ya sasa imeshafunguka ubongo na ina ufahamu mwingi sana. Wagombea wote (wa NGAZI zote) tuhakikishe kabla ya kwenda kuongea na watu kunadi sera zetu tuwe na uhakika wa sera zetu na tuwe na vipaumbele vinavyofikirika na kutekelezeka, vinginevyo tukienda majukwaani kuwananga watu tujiandae kushambuliwa kwa style zote za kijamii!

Mwisho: Cheo ni dhamana, na kama uliwahi kuwa nacho na HAUKUWAHI KUISAIDIA JAMII KWA JAMBO LOLOTE CHANYA, JIANDAE. Jamii ina kawaida ya Kulipa Fadhira!

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *