Kuna Sifa ambazo mtu akishakuwa nazo hafai tena kuwa kiongozi. Zipo Sifa mbovu za mbunge zinaweza kumyima nafasi ya kuendelea kuongoza zikiwemo:
Uzembe au kutokuwepo kazini bungeni. Mara nyingi Wabunge wa namna hii hutoroka vikao vya Bunge na kutumia muda mwingi kuzungukia wajumbe, na kuhonga makundi mbalimbali kwaajili ya kutafuta ushawishi jimboni.
Rushwa na ufisadi. Matumizi ya fedha, ugawaji wa Zawadi na matumizi ya mafungu ya mfuko wa Jimbo kwa mambo yake binafsi
Kutowajibika kwa wananchi waliomchagua. Kuwatenga Wananchi,kuwakwepa wasio mashabiki wake na kususa.
Kukosa uadilifu au kujitolea kwa maslahi ya umma. Uadilifu ni suala muhimu sana. Swali hili nawaachia Wananchi wajibu.
Kukosa uwezo wa kusimamia masuala muhimu au kushindwa kuwakilisha maslahi ya wananchi. Hili pia
Kwa ujumla, mbunge mwenye sifa mbovu ni yule ambaye hawezi kutimiza wajibu wake ipasavyo na ambaye hana uadilifu na uwajibikaji kwa wananchi wake na nchi kwa ujumla.