Imekuwa ni desturi ya muda mrefu kwamba kila aliye na hoja dhidi ya mafanikio ya Taifa la Tanzania anapigwa vikali na vigogo walioko kwenye mifumo wanaotegemea kunufaika na hoja hiyo.
Hofu, mashaka, vitisho, ujinga pamoja na umasikini vimekuwa ni tishio kwa vijana wa kitanzania kiasi cha kubana fikra zao kuelezea maslahi yao kwa taifa letu pendwa la Tanzania. Mfumo wa kiutawala ambao umekuwa ukidhoofisha mfunguko wa mawazo na fikra chanya kutoka kwa vijana wa kitanzania unachagizwa na uchu wa Madaraka pamoja na ufisadi wa watumishi wachache ndani ya Nchi yetu wanaolinda maslahi yao wachache huku wakitupilia mbali maslahi ya waliowengi.
UFIKE WAKATI SASA, watanzania wote tutambue kuwa fikra huru huliinua taifa. Hakuna taifa linaloweza kufanikiwa kwa kuwafanya vibaraka (machawa) vijana wake. Kuwazuia vijana kufikiria kisawasawa kwa maslahi ya Taifa lao ni kuwakosea sana na kulidumaza taifa.
Maisha ya Mtanzania wa sasa yanapaswa kuaksi uhalsia wa maisha ya vijana wa Kenya kwasasa. Watanzania wasiruhusu vijana kuwalamba miguu watawala ili kupata chochote. Lakini pia tusiruhusu suala la ukosefu wa ajira kugeuka kuwa kiboko cha kuwachapia vijana. Hii haitatusaidia na badala yake taifa litaangamia bila kupata msaada wowote kutoka kwa vijana kama sehemu kubwa ya nguvu kazi katika taifa hili.
Vijana huinua Taifa! Vijana ni Hazina kuu!