Mwelekeo wa Udiwani, Kata ya Kabanga

By admin May 12, 2025
Kabanga Imenoga, Kabanga ya wajanja; Kabanga yenye maendeleo ni manufaa kwa kila mkazi wa Kabanga. Pichani ni vinara vya kisiasa Kata ya Ngara na ni mmoja wapo kati yao atakayeiwakilisha kata hiyo kama Diwani. Nao ni Said, Hamim, na Hafidhi. Soma makala hii hadi mwisho ujifunze mengi.

Karibuni jamani nyumbani kwani Kabanga ni nyumbani kwa watu wengi wenye majina yaliyoshiba na yenye hadhi. Kabanga ni mji wenye ramani kama kiatu, kajimji kalikobeba vijiji vyote na kufunika majina yao kwani msanyiko wa hivyo vijiji vyote ninatengeneza kitu tunachoita Kata ya Kabang. Hawa wana kabanga, kama ramani yao ndio kiatu cha Wilaya ya utajiri kwani mapato mengi ya Halimshauri inakusanywa ndani ya Kabanga. Kwa uwezo wa kiuchumi, diwani anayotka Kata ya Kabanga ni mtu mzito sana kiwilaya na pengine hata kimkoa.

Ramani ya mji wa Kabanga unavyoonekana kutoka kwenye Sateraiti. Ramani ya mji wa Kabanga unafanana na sori ya kiato na ikiunganishwa na vijiji viliouzunguka huu muda vinatengeneza Kata ya Kabanga. Kulingana na tafiti, Kata ya Kabanga nyumbani mwa watu wasiopungua elfu 45.

Sasa palipokua na pesa kuna wajanja wengi na penye wajanja wengi, maendeleo hayakosekani. Wakati habari za chini kwa chini zinakusanywa, ilikua ni ngumu kuja na vinara wanaoweza kuongoza Kata ya Kabanga. Ilikua ni ngumu kupata uhakika kuwa wanaotajwa kama tatu bora kwenye sakata la udiwani, kweli watanyakua hadhi ya kuwakilisha hii Kata kwani wana Kabanga wengi wanaishi nje ya Kata na muda mwingine nje ya Wilaya ya Ngara. Tumeamua kuelekeza macho kwa wale wanaoishi Kabanga ingawa mwana Kabanga yoyote anaweza fukuza uvivu na kuingia kwenye uringo ili awakilishe Kata yake ya Kabanga kwenye baraza la Madiwani.

Tuanze kwa kutambua mchango mkubwa na uadilifu mkubwa Diwani aliyepo madarakani aliofanyia Kata ya Kabanga, Mheshimiwa Hafidh Abdala. Mheshimiwa Abdala ndie nahodha kwenye hili sakata kwani ndie kwa sasa amelivaa koti la heshima ya kuwakilisha Kata ya Kabanga kwenye baraza la Udiwani. Hajaisusa Kata yake na hakika hatosogezwa pembeni kiuvivu vivu. Kwa hiyo mnaokodolea macho udiwani wa Kabanga, basi muwe mmejiandaa kweli kweli.

Kulingana na tafiti zetu hapa Kababanga, majina maarufu yaliyojitokeza kama majogoo wanaoweza kung’oana meno katika ulingo wa siasa ni Mheshimiwa Hafidh Abdala na Ndugu Hamim Baruani.

Historia yao inaanzia kipindi cha Uchaguzi mkuu uliopita, ambapo kinyang’anyiro kilikuwa kikali sana na hatimae Hafidh akafanikiwa kunyakua ushindi. Kwa sababu muda umepita na wote bado ni vijana, je Ndugu Hamim Baruani ataweza kumsogeza pembeni diwani aliyepo madarakani? Kwa kweli hili tuwaachie wakazi wa Kabanga waliamue.

Jina la Said Soud maarufu zaidi kama Said Mnene sio geni! Kwa sasa ni Mheshimiwa diwani mstaafu. Ndie aliemuachia kiti Hafidh. Hapa mtaani vijiweni wanamtaja kama anataka kugombea tena. Swali ni je, atafanikiwa kurudi ama pengine ataendelea kucheza na wajukuu na kufurahia maisha yasiyokuwa na purukushani za kisiasa hususani muda huu ambabpo upepo wa vijana unatikisha tikisa kila tawi linalojaribu kuingia katika ulingo wa Siasa?

Kundi kubwa la vijana bado wanaamini sana katika uwakilishi wa vijana wenzao hasa katika kuleta mawazo mapya na ubunifu kwani katika watu watano siku hizi hapa Kabanga, basi wanne wana smart phone (simu janja) na kama inakupatia changamoto kuitumia ama unaiwasha kama redio – pale unapotaka kuitumia tuu, basi tena jua changamoto zinazokumba vijana hautoweza kuzitatua. Utaona matakwa ya kisiasa kama ni bugudhi na makelele tuu. Utaishia kufikiria kila anayetaka mambo mapya ama ubunifu ni mpinzani ingawa anaweza kuwa amevaa sare ya chama chako.

Vijana mara nyingi wana mtazamo mpya kuhusu changamoto za kijamii na wanaweza kuibua suluhisho mbadala kwa kutumia teknolojia na ubunifu. Hapa Wilayani, vitu vingi na matamanio mengi ya vijana hayafanikiwi kwa kutokuwepo viongozi wanaweza kwenda na kasi ya kimaendeleo. Juhudi zao zinaangushwa na viongozi ambao wanajitamba kwa kuwa na majina maarufu, umarufu uliozaa umasikini uliopo. Kutwanga kitu kile kile kilichoperekea wananchi kuwa mafukara ni mchezo vijana wengi wameona wausogeze pembeni ili kuwepo maisha nafuu.

Kama kijana hapa Kabanga anaweza kutumia internet na kuweka order ya vitu kutoka Japan na vikafika, kweli kiongozi ambaye anatumia kitochi cha mchina atatusaidia chochote? Mtu ambaye akipewa jambi aanike mafanikio yake anaishia kukimbilia mahakamani kulia lia, huyo naye ataongoza nini, wapinga tunguri ama mbio za mahakamani akiwa amevalia koti ambalo halijafuliwa miezi nenda rudi, aliuliza binti wa Kabanga? Kabanga inahitaji kiongozi mwenye sifa za ubunge, mtu ambaye akitoka hata nje ya wilaya basi hatoonekana ni kituko ama mcheza sengeri, aliongezea mkazi wa Kabanga aliytaka kujitambulisha kama mfuga Manguruwe. Tunataka shule na visima vinavyotoa maji na sio hivi visima ambavyo baada ya kujengwa havihudumii jamii kwa zaidi ya miezi sita, aliongezea makazi ambaye alitaka kujulikana kama Uongozi Si Fitina. Kama mradi hautoanza kuhudumia jamii unapoletwa, basi waache kujenga vitu vinavyoishia kukusanya vumbi, aliongezea Uongozi si Jina na akaongezea eti “tunataka vijana waongoze kwani technologia imetusogeza na ulimwengu na aliyepigwa teke na technolojia aendelee kunufaishwa na ubobezi wa vijana katika uongozi. Tunataka tuweze kuchungulia yanayofanywa na wengine ili angalau nasi tuige”.

Kuwakilisha maslahi ya vijana wenzao: Wanapokuwa madiwani, wanaweza kuhakikisha kuwa mipango ya maendeleo ya mtaa inazingatia mahitaji ya vijana kama vile ajira, elimu, michezo, na afya ya akili. Ajira na elimu zitaboreshwa na uwepo na uelewa wa matumizi ya technolojia. Vijana wanahitaji “skills” ili wapate pato la kujenga kwao na kutunza familia zao. Ndio, afya ya akili inaweza adhirika kutokana na matumizi mengi ya technolojia ila wa uchumi wana Ngara, uwepo wa wabobezi wa afya kwenye hizi simu utasaidia wengi katika kusambaza elimu na huduma mbali mbali haswa ule wa afya.

Kuchochea ushirikishwaji wa jamii: Vijana wanaweza kutumia nguvu na ushawishi wao kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo kama mikutano ya kijiji, ujenzi wa miradi ya pamoja, na usafi wa mazingira. Vijana wanaweza kuwa walinzi wa jamii kwa kupewa fursa katika ulinzi, kusaidia kujenga visima, mitalo, vyoo, na kadharika kwani fedha zinazokuja kujenga haya mambo yanaishia kwenye mikono ya wenye ukaribu na wale wanaoitwa watu wa juu. Kwa kutumia uwepo wa media, vijana wanaweza kuonyesha changamoto zilizopo na viongozi husika kuzishughulikia ama hata wale wa juu kuona kinachoendelea na kutenga ufuko ili changamoto itatuliwe kwa uharaka. Matumizi ya teknolojia za kisasa vijana wengi wanaamsha viongozi na kuweka msisitizo wa lipi limesahaurika ama lipi linakwamisha mission zao.

Kuimarisha uwajibikaji: Wakiwa viongozi, vijana wanaweza kuhimiza uwazi katika matumizi ya rasilimali za umma na kusimamia utekelezaji wa miradi kwa uadilifu. Vijana wakiwa katika uongozi, changamoto wanazigeuza kama fursa na sio kudai wameabishwa. Jambo linashughulikiwa kwa uharaka kwani teknolojia imeshageuza vijiji kuwa miji hasa ukilinganisha jinsi wana Ngara hata wakiwa nje ya wilaya wanashiriki kikamilifu katika kutoa michango ili jambo lishughulikiwe. Hata watoto kadhaa hapa kwenye kata wameshanufaika kwa kupata wafadhili, matibabu na kadharika pale changamoto zao zilipoanikwa hadharani. Zamani bila uwepo wa teknolojia, changamoto zilikua zinaonwa kama laana ambazo ni za kufichwa na si kutatuliwa.

Kkwa kusisitiza tena; kukuza teknolojia na mawasiliano: Vijana wanauelewa mkubwa wa teknolojia, na wanaweza kutumia mitandao ya kijamii au majukwaa mengine ya kidijitali kushirikisha wananchi na kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya eneo. Kwa kutumia technolojia na masiliano, hatuna cha kupoteza zaidi ya ushamba na ujinga. Hamna mwenye hati miliki na uongozi, wilaya, kata na hata mtaa. Kila mtanzania mwenye sifa anaweza kutuletea mchango chanya wa kimaendeleo hususani baada ya kutembea na kuona yanayoendelea sehemu nyingine. Kama aliongezea shule ama alikusanya ujuzi kwenye harakati za kutafuta, umarufu wa jina, kabila, dini, umri ama jinsia si vigezo tena vya kumnyima mtu fursa ya kuongoza ama kuleta maendeleo kwenye jimbo lake. Vijana ni wa elewa na wanajua mengi na wanaweza kukinzana na pirika pirika za jana na leo ila ni jema litakalotokea watakaposhirikishwa.

Utafiti ulionyesha kuwa baadhi ya wana Kabanga wanaridhishwa na utendaji wa Mheshimiwa Hafidhi na wameahidi kumuongezea muda Mheshimiwa Hafidh ili atimize ahadi zake alizoanza kutekeleza, na wengine wanaoona kuna umuhimu wa kumjaribu kijana mwingine.

Vile vile wapo wazee wanaoona kuna umuhimu wa kumtafuta mzee mwenzao kwa kuwa vijana wana vurugu. Wamedai uzee haumnyimi mtu uwezo wa kutumia technolojia. Wazee wengi wana uelewa na wanaweza kutumia technolojia mbali mbali hususani software za maofisini. Wazee wana ushawishi mkubwa tuu hata huko serikalini kwani wana busara nyingi ambazo zinahitajika katika kufanya maamuzi kwa manufaa ya wengi. Mvi ama utaratibu katika kufanya maamuzi sio kwamba yatakayoamuliwa ni mabaya. Ni vizuri changamoto zijadiliwe, zipimwe, na uamuzi ufanyike kwa manufaa ya jamii kwani kukurupuka si jambo jema. Swala la kisiasa haliamuliwi na mtu mmoja, mzee Nyabyoba alisema. Jambo linajadiliwa katika kamati na muda mwingi kiongozi anakuja kubariki tuu baada ya kutafakari na kuona manufaa yatakayopatikana kwa jimbo na watu anaowaongoza.

Sifa za wagombea 3.

Mheshimiwa Hafidhi Abdula, Diwani wa Kabanga

1. Hafidh Abdala, Diwani wa sasa amejtahidi kwa kwa kiasi chake. Ametimiza ahadi na kujitolea kwa hali na mali kusaidia wananchi.

Wakati mwingine hutumia hata fedha zake mwenyewe, kusaidia makundi mbalimbali ya wananchi nk. Kiuchumi yuko vizuri 

Ndugu Hamim Baruani

2. Hamim Baruani, huyu ni kijana machachari na mbichi kabisa ambae amekulia katika misingi ya Chama cha Mapinduzi. Muadirifu na anaijua Siasa sawa sawa. Kifedha ni mtu wa kawaida, anafaa kuongoza ila anatajwa kuwa muumini na mfuasi wa wanasiasa(CHAWA). Kwa Siasa za Ngara, uchawa umeharibu heshima na sifa za Ngara iliyojengwa na wazee. Uchawa na unafiki ndio uliozaa umasikini unaoponza watu wengi leo.

Ndugu Said Soud

3. Said Soud, Mkongwe na mzoefu wa Siasa. Huyu ni baba, mjomba, na pengine babu kwa wana Kabanga wengi. Kwa wana Kabanga wengi, Mheshimiwa Said ni mjomba kwani amesaidia watoto wengi kwa kuwavusha bara bara ama hata kuwapatia lift kwenye gari lake. Ila kama mlizi wa jamii, anasifika kuwa mkali na kutopakata uvivu ama utoro mashuleni kwa vijana. Kuna watu walikua wanamuogopa huyu mjomba kwani akikasirika alikua anakutishia pisto/ bunduki kwani ana historia ya TRA/upolisi. Ila alitumia ukali kutia nidhamu watu wengi na kama mzazi ni muhimu sheria na taratibu zilizowekwa zizingatiwe na kuheshimiwa. Kwa kifupi Mheshimiwa Said ni kama kochi kwa watu wengi kwani nia yake ni kuona mafanikio wa watu wengi.

Ni Mtu mzima na mwenye kipato. Anatajwa kugombea na huenda akifanikiwa kurejea kwenye Uidiwani akasahihisha makosa yake ya zamani.

Ukweli ni kwamba, sasa Kabanga inogire! Kuna majina mengi mengi ya wana Kabanga ambayo yametajwa ila kutokana na kutokua na ukazi endelevu kwa hapa Kabanga, ni ngumu sana kuja kung’oa mmoja wa hawa vinara waliotaja ila yote yapo mikononi mwa wakazi wa Kata ya Kabanga.

Kwa kifupi, wana Kabanga, Kazi kwenu Wananchi. Tunakaribisha comments zenu hapa chini. Tunapenda kuelekezwa, kukosolewa, na kufunzwa. Nia yetu ni kutoa habari bila kuegemea upande fulani na kama kuna aliyesahaurika, basi weka majina yake hapa kwani tumekusanya hayo yalioandikwa baada ya kuzungumza na wanahusika. Tunashukuru kwa kuendelea kuwa nasi. Ngara imara, na Kabanga Moja Yenye Upendo ni faida kwa kila mwana Kabanga na Ngara kwa kiujumla.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *