Udiwani Kata ya kanazi ni Kaa la Moto

By admin May 5, 2025
Pichani, Nuru Nzoya kijana machachari akifanyiwa mahojiano na moja ya Luninga nchini Tanzania, picha nyingine ni Mugatha kushoto ambaye aliwahi kuwa Diwani Kanazi, na kulia ni mwalimu na afisa elimu mstaafu mzee Sitini diwani wa sasa

Na, Bankanzako Ruguna

Kanazi-Ngara

Ni mtifuano usio wa kawaida kwa mujibu wa utabiri wa wananchi wa kata ya Kanazi kuelekea Uchaguzi mkuu. Kata yenye kila aina ya sifa ya Uongozi na Utawala.

Kuanzia utawala wa kichifu(Chifu Balamba) hadi Ubunge. Ndio kata inaongoza kwa kutoa wabunge wengi kuanzia Sebabili Gwasa,Gachocha na Ruhoro.

Kuelekea kura za maoni ndani ya Chama cha mapinduzi katani humo tayari vinywa vya wenye kata vinawataja baadhi ya watia nia wakiwemo……..

Mathias Mugatha – Diwani mstaafu aliyeiongoza kata ya Kanazi kwa miaka 20.

Sitini Rugana – Diwani anayemalizia muda wake. na

Nuru Nzoya – Kijana msomi na mjuzi wa mambo anayewania kiti hicho kwa mara ya kwanza.

Wakati kibarua kikisukumwa kwa wapiga kura tayari utabiri umeanza huku likiwepo kundi linalomtaka diwani kijana na mpya, na likiwepo pia lingine linalotaka kuona miamba miwili Sitini ambae ni diwani wa sasa akitoana jasho na Mugatha diwani wa zamani.

Duru za kisiasa zinaeleza kuwa upande wa Mugatha unayo  nafasi ya kufanikiwa kwakuwa unaungwa mkono na mbunge wa sasa Ruhoro Ndaisaba.

Kwa mujibu wa taarifa hizo ni kwamba  Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba, hamuungi mkono Nuru Nzoya katika kinyang’anyiro hiki kwasababu ya kuogopa kugombana na mratibu wake ambae ni Mugatha. Swali ni Je, Wananchi washindwe kupata uwakilishi wa mtu wanaompenda kwakuchaguliwa diwani na mbunge?

Wapo wanaomfahamu Mugatha kwa uwakilishi wake muda mrefu alioiongoza kata ya Kanazi, shughuli zake mazuri na mabaya! Watajua la kufanya. Mbu ge asiwaingilie.

Wapo wanaomfahamu na bila shaka kama kuna makosa ya diwani wa sasa afisa elimu mstaafu wanayaona na mazuri pia, waachiwe wenyewe wafanye maamuzi.

Nuru Nzoya bado ni kijana. Kama alivyoingia Bungeni mbunge akiwa kijana, ni wakati wa Kanaxi sasa kupata Diwani kijana . Mbunge aache kuogopa vijana badala yake aungane nao waunganishe nguvu na kuiongoza Ngara. Aliwahi kunukuliwa akimwambia kijana mmoja mtia nia kata moja wapo ya tarafa ya Murusagamba kwanba hatatoboa….kauli ya kukatisha tamaa.

Nuru ni kati ya waliomsafishia njia ya mafanikio mbunge. Alizunguka jimbo usiku na mchana,alivuka hatari nyingi kuhakikisha anawezesha ushindi.

Kwa kigezo cha Umri, Nuru ni kijana ambae atapambana na wazee. Je, Ushindi ni timu kijana au Wazee?

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *