MWALIKO WA ZIARA YA VIONGOZI WA CCM KATA KUZURU BUNGE KUTOKA KWA MBUNGE WA NGARA NI KOSA KWA MUJIBU WA KATIBA YA CCM YA MWAKA 1977 TOLEO LA 2022
Uchambuzi wa Kisiasa
Na:-
Mwandishi Wetu
JAMII inapaswa kutambua kuwa, Chama Cha Mapinduzi ndicho chama mama nchini Tanzania kilichoundwa Mwaka Mei 2, 1977 baada ya Muungano wa Tanganyika African Nation Union (TANU) kutoka Tanganyika (Tanzania bara) na Afro-Shiraz Party (ASP) kutoka Zanzibar.
Baada ya kuundwa kwa chama hicho, iliundwa misingi mbalimbali ya kuweza kutawala chama hicho (viongozi na wanachama) hadi ikapelekea kuundwa la katiba ya CCM ya Mwaka 1977.
Katiba hii ya CCM ya 1977 imepitia marekebisho mengi (matoleo) lengo ikiwa ni kuimarisha misingi na kuweka upatinishi kati ya watawala na watawaliwa ndani ya chama hicho.
Katiba ya CCM imerekebishwa mara 17 katika matoleo tofauti kama ifuatavyo:-
- Toleo la 1980
- Toleo la 1982
- Toleo la 1984
- Toleo la 1987
- Toleo la 1990
- Toleo la Machi 1992
- Toleo la Septemba 1992
- Toleo la 1994
- Toleo la 1995
- Toleo la 1997
- Toleo la 2005
- Toleo la 2007
- Toleo la 2012
- Toleo la 2017
- Toleo la 2020
- Toleo la Aprili
2022 - Toleo la Desemba 2022
MBUNGE wa NGARA Ndugu NDAISABA GEORGE RUHORO anapaswa kusoma vizuri Katiba ya CCM (chama kilichompa dhamana) kabla hajaamua jambo lolote lenye mahusiano ya moja kwa moja na uongozi wa chama (CCM) Ngazi ya wilaya.
Kwa Mujibu wa Ibara ya 17 (1&2) ya Katiba ya CCM ya 1977 Toleo la 2022 kiongozi anapaswa kuwa mtu aliyetosheka na asiwe mtu aliyetawaliwa na tamaa, lakini pia awe ni mtu anayependa kueneza Matunda ya Uhuru kwa wananchi wote kwa manufaa yao na kwaajili ya Maendeleo ya Taifa kwa jumla.
Hao viongozi wa CCM wa kata za Ngara hawazuiliwi kuhudhuria bungeni kama watu huru kwa majina yao ila kuhudhuria bungeni kwa mwaliko wa Mbunge wa Ngara kwa utambulisho wa vyeo vyao ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya kata inavunja Katiba ya CCM na inatia doa menejimenti nzima ya chama wilaya kwa kibali watakachokitoa kwa viongozi wao hao wa chini (ngazi ya kata).
Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 Toleo la Mwaka 2022 chini ya Ibara ya 15 imeeleza maana ya kiongozi ndani ya CCM. Lakini pia Ibara ya 17(2) imewapa mamlaka viongozi wote kueneza Matunda ya Uhuru kwa wananchi wote, na hapo tunaona Mbunge wa Ngara ambaye pia anategemea Uhuru wa viongozi hao wa kata uamue katika kura za maoni kwenye teuzi zijazo (na Mbunge akiwa moja wa watiania) CHAMA HAKIONI KAMA kuwaruhusu viongozi wa Kata kwenda Bungeni kwa tiketi ya vyeo vyao Tena kwa mwaliko wa Mbunge NI KUUZA UHURU WAO WA KUENEZA MATUNDA YA CHAMA CHAO kwenye jamii ?
Chama cha Mapinduzi (CCM) NGARA, kinapaswa kutafakari yafuatayo:-
- Kwanini viongozi wa kata waalikwe sasahivi mwaka mmoja kabla ya kukoma kwa ubunge wa Mbunge wa sasa wa Ngara?
- Mwaka 2020, 2021, 2022, na 2023 hakuona umuhimu wa kuwaalika viongozi hao wa kata hadi awaalike mwaka huu ?
- Kwa Mujibu wa Katiba ya CCM viongozi wa kata huongozwa na maelekezo kutoka uongozi wa CCM wilaya. Je uongozi wa CCM wilaya ya Ngara unadhani ni sahihi kuwaruhusu viongozi wa kata kuhudhuria mwaliko wa Mbunge wa Ngara kwa sasa kwa mujibu wa Katiba yao ?
- Je utapatikana wapi uhuru wa kisiasa ndani ya CCM kama mmoja wa watu (Hon. Ndaisaba) wenye kufaidi uhuru jumuishi wa viongozi wa chama kwa ngazi zote atapewa ridhaa ya kuonana na viongozi wa chama wa ngazi ya kata kipindi hiki chama kinapoelekea kwenye maandalizi ya chaguzi za 2024/2025?
- Je Chama cha Mapinduzi (CCM) NGARA kinataka kuiaminisha jamii na kuutangazia umma kwamba kila mwenye nia na ubunge wa Ngara yuko huru kujihudhurisha na kuwahudhurisha VIONGOZI WA chama kwa ngazi yoyote kadri anavyoona inamfaa bila kuzingatia kanuni na katiba ya chama ili kujiongezea ukubalifu ?
Rekodi zinaonyesha wazi kuwa Mbunge wa Ngara kupitia tiketi ya CCM Ndugu Ndaisaba George RUHORO amewahi kuwahonga Tsh 50,000/= viongozi wa CCM wa kata za Ngara kama sehemu ya posho (hela) ya sikukuu kama walivyoeleza wanufaika kitu ambacho ni kosa kikanuni na kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Leo anawaita kwenda Bungeni DODOMA, chama kikitoa kibali hicho kitakuwa kimejihakikishia kwa asilimia ngapi kwamba ziara hiyo ya viongozi wa kata (CCM) ni salama kwa ustawi wa chama hicho ngazi ya wilaya ? Na je mtu akisema CHAMA CHA MAPINDUZI Ngara kinamilikiwa kwa miongozo na matwaka ya Ruhoro atakuwa anakosea ?
CCM NGARA ni Mali ya WANACCM WOTE.
MBUNGE WA NGARA ASITUPOTEZEE MSTAKABALI.
VIONGOZI WA CHAMA SIMAMENI IMARA, HIZI AIBU NI KUBWA MNO!