Joto la Uchaguzi 2025 Lazidi Kumpagawisha Mbunge wa Ngara

By admin May 22, 2024
Mhe George Ruhoro: Baada ya kuhisi kijiti cha kuiwakilisha Ngara kukaribia kumponyoka. Ruhoro Aja na Mbinu Mpya: Ajikomba Kuwa Kiongozi wa Koo zisizo zake, za kiuchifu ili aendlee kuwa relevant kwenye siasa.

Na: Parc princes 

Kila Siku Anabuni Mbinu za Ushindi, Nyingine ni Chafu – Hazifai!

KILA SIKU ANABUNI MBINU ZA USHINDI, NYINGINE NI CHAFU HAZIFAI.

Katika kile kinachoashiria hofu ya kupoteza Umaarufu wake kutokana na mbinu chafu anazozitumia kuwahadaa Wananchi kwa lengo la kujipatia Umaarufu na kuwashika wapiga kura Mbunge wangu Sasa Bora uachane na Siasa ujikite kwenye Biashara ili usipoteze mwelekeo. 

“Kwakuwa ulishatueleza kuwa huna mpango wa kufilisika wala kuwa masikini kana kwamba una maagano na Mungu basi nikushauri tu uachane na Siasa ambazo zinakutoa kwenye msitari kila siku huku ukibuni mbinu za tamaa ili ubaki kwenye Utawala,hakika unatia mashaka.” Ushauri wa mmoja Mpiga kura

Mbunge wa Jimbo la Ngara Ndaisaba George Ruhoro tangu alipotangazwa kuwa mshindi Katika Uchaguzi wa 2020 amekuwa Mbunge wa kwanza kuwa na mbinu chafu anazotaka zimtengenezee historia ya kujirudia Katika USHINDI kwenye Uchaguzi ujao.

Inaelezwa kuwa tangu amechaguliwa amekuwa mtu wa matukio mengine ya kuistaajabisha Ngara,hata Tanzania likiwemo la kurubuni baadhi ya wakuu wa familia na Koo kumpa nafasi ya kuwa Mlezi wao.

Licha ya kuwa Utawala wa Kichifu ulifutwa na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika na Baba wa Taifa la Tanzania Mwl. J.K Nyerere, Mheshimiwa Ndaisaba anautaka!.

Inaelezwa pia, amekuwa Mbunge wa kwanza kulazimisha Umaarufu kwakuwalazimisha wafanyabiashara wa Wilaya hii yenye historia ya kuzalisha Viongozi wenye heshima Tanzania,watu maarufu na nguzo za Taifa kubandika Picha zake kutani,kwenye maduka na kuzipamba ndani ya nyumba zao kujifananisha na Rais.

…”Ndiyo, kijana wetu amelewa madaraka hata vijana wake wapambe wanaimba mitano tena unafikiri maana yake nini, we hujasikia?” Mzee mmoja kutoka kijijini Katerere kwao na Mheshimiwa.

Akisimulia kwa masikitiko Mzee huyo anaeonekana kumfahamu vizuri Mheshimiwa Mbunge alisema ni kizazi cha aibu na fedheha kinachoweza kutamani kujilinganisha na Mheshimiwa Rais, na kudharau wazee wakiwemo watangulizi wake Katika kiti cha Ubunge.

Matukio mengine yanayotajwa kuwa mbinu chafu anazotumia Mheshimiwa kuitafuta Umaarufu ni pamoja na 

1. Kauli za dharau kwa Wananchi kuhusu UTAJIRI. Anawatambia wapigakura wake kuwa anamiliki Makampuni zaidi ya 7 yanayomtengenezea mabilioni ya fedha kila siku,hivyo Hana mpango wa kufilisika anamiliki magari na nyumba za kifahari.

2. Anaetaka Ubunge wa Ngara 2025 labda ajipange Kuja na fedha taslimu shilingi Bilioni 3 na kuendelea.  Hii inamaana kwamba amejiwwka sawasawa kutumia Pesa kuhakikisha anatetea nafasi yake.  Mwl. Nyerere aliwahi kutahadharisha mtu anaetumia Pesa kutafuta UONGOZI huyo ni wa kutiliwa mashaka. Je, Kiburi hicho Mheshimiwa Ndaisaba anakipata wapi?

3. Kutumia Vijana kuvuruga Amani ya Wilaya kwa Usumbufu mitandaoni,kuzua taharuki kwa kutukana wazee na kubeza utendaji wa waliowahi kuwa Wabunge. Kupitia makundi sogozi ya mitandao hasa Whatsapp groups umekuwa kawaida kila siku kushuhudia dharau za vijana wanaotajwa kuwa genge lake wengi wakitajwa kulipwa fedha na kuzawadiwa vitu mbalimbali yakiwemo magari kuchafua watu,kubeza na Kutoa vitisho kwa watu wanaoonesha Nia ya kumkosoa bosi wao hadharani. 

4. Hivi karibuni, imeibuka minong’ono ya matumizi mabaya ya Ofisi ya Ubunge. Tunatambua kuwa Ubunge ni Taasisi. Mkuu wa Taasisi anatakiwa kuwa mfano wa Maadili mema! Minong’ono inahusisha tabia mbaya ya kutembea na wasichana,kuwazalisha na kuwatelekeza.

5. Kutumia nafasi yake kuhalalisha uraia wa baadhi ya watu wanaoonekana kumnufaisha.(Raia wa Rwanda na Burundi Katika Biashara,mifugo,ngono n.k).

6.Kuingilia Tume ya Uchaguzi. Ni kinyume na taratibu  za Uchaguzi,na mara kadhaa Viongozi wa Chama wamesema juu ya hilo Katika kile kinachotajwa kujipitishapitisha…..

-Mheshimiwa Ndaisaba ndiye kinara wa uvunjaji wa Sheria. Mratibu wake mmoja aitwae Mgatha na wapambe wake kila siku wako field kuratibu na kupanga watu watakaogombea nafasi za Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.

-Kana kwamba hiyo haitoshi, anaratibu na kuwapanga wagombea Udiwani wa 2025 ili kupata unafuu atakapogombea. 

5. Mpango wa kumtengenezea nafasi mratibu wake kuwa Diwani wa Kata ya Kanazi,na baadae aje kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri baadae. Hili liko wazi, na baadhi ya Madiwani wameshaliona.

6. Kuwachonganisha Madiwani na Wananchi. Kila zuri,fanikio au Utekelezaji kwenye Kata anasema ni jitihada zake. Hali hii inadhoofisha uwakilishi wa Madiwani hasa wenye msimamo na kumkosoa hadharani.

7. Kubeza utendaji wa Wabunge wa zamani. Aliwahi kusikika akisema mafanikio yote yanayoonekana Ngara hasa Miradi ya Maji,Umeme,Afya na miundombinu ya Barabara na Mawasiliano ni matokeo yake kwani Wabunge waliotangulia walikuwa wa kusinzia Bungeni tu. Hilo linatajwa kuwa ni kashfa kwa wazee.

Maswali yanayoulizwa na Wananchi ni je,?

Kama kila kitu linafanywa na Ndaisaba, je Serikali kuu haipo? Mkuu wa Wilaya anafanya nini?

Chama kilichompa ridhaa hakikuwahi kutekeleza Ilani kabla yake?

Halmashauri haipo?

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *