Police State ama ni State Police?

By admin Apr 11, 2025
Police State!!  Ama state police.... Tofauti ni zipi... State Police ni jeshi la Police ambao wanalinda taifa ila pale tunapokua na police state ni pale police wanapotumiwa kulinda chama fulani na si kwa manufaa ya taifa. Jeshi halifai kulinda matakwa ya watu fulani bali inatakiwa kulinda taifa kwa ujumla bila kujali kibila, dini, wala viashilia vyovyote vya kibaguzi. Je, ni hali ipi inayotokea hapa kwetu, Tanzania.

Na Sam Ruhuza

Hii hutokea pale Rungu linatumika kuipiga HOJA! 

Wanasiasa hubishana kwa hoja kujenga usahihi wa kueleweka, mfano hivi karibuni kiongozi mmoja wa chama tawala alidai kuna chama kimejipanga kununua virus vya ugonjwa hatari kuvisambaza nchini ili watu waugue na hivyo kuahirishwa uchaguzi mkuu!! 

Japo aliongea mkutanoni kwa kujiamini sana, lakini maneno yake yalipuuzwa na kuchukuliwa kama lugha za Wanasiasa katika kujenga hoja kukubalika! Police wala hawakumsumbua kwa uchochezi!! 

Kauli nyingi zimekuwa zikitolewa na viongozi wa chama tawala sehemu mbalimbali za kuhamasisha vijana kupambana na wapinzani na wengine hata kuomba Police wasiingilie, lakini Police hawakuwakamata wala hata kuwaonya kwa uchochezi kwasababu walichukulia ni kauli za kisiasa! 

Hivi karibuni Chadema imekuwa na ksuli yao ya No Reform, No Election ambayo wanatoa hoja yao ya kuhamasisha wananchi wasikubali kuingia kwenye uchaguzi mkuu 2025 hadi mabadiliko yanayohusu uchaguzi yafanyike ikiwamo Tume Huru ya Uchaguzi na wamekuwa wakitoa ufafanuzi wa wazi kuhusiana na hoja yao hiyo ambapo kwa kiasi fulani imepokelewa kwa mitazamo tofauti na wananchi huku wengine wakitaka kupata ufafanuzi zaidi. 

Chama tawala pamoja na baadhi ya vyama wamekuwa nao wakihamasisha ushiriki wa uchaguzi mkuu 2025 kwa hoja zao! 

Kwenye siasa mnabishana kwa Hoja!  

Huo mjadala ulikuwa mzuri sana ambapo umeweza kusaidia wapiga kura umuhimu wa kura zao,hivyo imesaidia kutoa Elimu ya uchaguzi. 

Jana na leo hali imebadilika baada ya Police kumkamata Mkiti Chadema Tundu Lissu na kumfikisha Mahakama kwa kosa la Uhaini! Pia kuna taarifa mitandaoni za kupigwa mabomu ya machozi ofisi za Chadema na hata kukamatwa baadhi ya viongozi wakiwemo Makamu Mkiti John Heche!  

Sababu kubwa ikidaiwa ni uchochezi wa kuhamasisha wananchi kususia uchaguzi mkuu! 

Sina hakika na uelewa wangu mdogo kuhusu tafsiri ya Uchochezi na Uhaini! 

Nakumbuka wakati nasoma shule ilikuwa ukisikia Uhaini au mtu mhaini, duuh! Unashtuka mno na ilikuwa ni ngumu sana kusikia ameshtakiwa kwa kosa hilo unless wanajeshi wamehusika, maana ni Mapinduzi hayo, lakini siku inaanza kuzoeleka kwa Wanasiasa kupewa kesi za Uhaini!! 

Kipindi cha JK aliwahi kusema, anatamani kuifanya chama chake kijiendeshe kama chama cha siasa kwamaana ya kutokuishi kwa kutumia Dola, baada ya kuona matumizi ya kamata kamata, akawataka wanachama wenzake wawe wanajibu hoja kwa hoja na sio kulalamika tu kutaka watu kukamatwa! 

Bahati mbaya sana baada ya kuondoka kwake 2015, imekuwa ni matumizi hayo ya mabomu na kamata kamata! 

Mwaka 2021 Rais Samia alipoingia madarakani alisema anataka 4Rs (Reconciliation, Resilience, Reform and Rebuild) ndizo ziendeshe Kipindi chake! 

Mabadiliko aliyoyafanya alipoingia madarakani, alivuta hisia kubwa za watu wengi na kuaminika sana, lakini baadae hizo 4Rs ukiziulizia, hata wenyewe hawazisemi tena!! 

Resilience (uvumilivu) hasa wa kusikiliza usichopenda kama kukosolewa ndio imekuwa mtihani mkubwa sana kwa mtawala! 

Watanzania ni wamoja mbele ya chochote kile kwamaana Taifa ndilo linakuja kwanza, hivi vyama vya siasa ni baadae kwenye kutaka madaraka na kuna nchi zinakwenda vizuri tu bila vyama vya siasa. Tulinde Taifa kwa kuepuka ushabiki wa kisiasa, mijadala iwe ya Hoja na sio kutumia nguvu za marungu, mabomu, kamata kamata, kesi,…! Hii hali inaamsha mengi yasiyofaa! 

Police ni chombo nyeti na muhimu sana kwa Taifa,  fikiria Taifa bila Police linakuwaje?! Police wana mambo mengi sana ya kulinda Raia na Mali zao,wapewe Uhuru huo wa kufanya kazi zao ili kulinda heshima yao. 

Wanasiasa wanaopenda kutumia madaraka yao kuingiza Police kuwasaidia kupambana na wapinzani ni kuwakosea sana na kuwaingiza katika mijadala ambayo hawapaswi kuwamo! 

Jeshi lilikuwapo, lipo na litaendelea kuwapo pasipokujalisha chama gani kipo madarakani, Wanasiasa wao wanabadilika kila mara, acheni vyombo vyetu vya Dola vifanye kazi yake kwa weledi bila kuingiliwa! 

Hivi vyeo vya Mkiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya/Mkoa kuendeshwa na Wanasiasa ndipo tatizo linapoanzia! 

Mheshimiwa Rais ingilia hili kutetea 4Rs zako maana naona huko tuendapo sipo! 

Kama kuna hoja za uchaguzi mkuu, zijibiwe kwa majibu sahihi, vinginevyo kaaeni msikilize muelewane, kuliko hiki kinachoendelea, hakina afya njema kwa uhai wa Taifa.  

Tunapenda Amani, tuongee bila fujo wala kupigana! 

Tanzania ni yetu sote! 🇹🇿🤝💪

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *