SALAMU ZA POLE

By Na Mwandishi Jun 16, 2026


Uongozi na wafanyakazi wa Ngara TV tunatoa pole za dhati kwa familia ya Ruhuza kufuatia kifo cha ndugu yao mpendwa, William Ruhuza, kilichotokea hivi karibuni.


Tunatambua kuwa kuondokewa na mpendwa ni pigo kubwa lenye maumivu na huzuni isiyoelezeka. Katika kipindi hiki kigumu, tunaungana nanyi katika maombi na kuwaombea muwe na nguvu, faraja na uvumilivu wa kuhimili msiba huu.


Tunamuomba Mwenyezi Mungu azidi kuwapa utulivu wa moyo wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu, na amsamehe marehemu dhambi zake zote pamoja na kumpumzisha mahali pema peponi.


“Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana lihimidiwe.”


Pumzika kwa amani, William Ruhuza.


Imetolewa na:
Uongozi na Wafanyakazi wa Ngara TV
www.ngaratv.com⁠