Ubunge Jimbo La Ngara Kama Tyson na Jake Paul

By admin Nov 16, 2024
Mike Tyson na Jake Paul wakichuana huko jijini Dalas Texas, November 15, 2024. Jake Paul aliibuka kuwa mshindi dhidi ya mpinzani wake.

Ni wazi kwamba homa ya Uchaguzi Jimbo la Ngara inazidi kupanda kila kukicha.

Lipo kundi la wanataka Ubunge wa mwakani,uchukuliwe na Wazee huku kundi lingine hasa la Vijana likitaka Vijana wawakilishwe na kijana mwenzao Katika mjengo.

Yapo majina ya baadhi ya wanasiasa maarufu Ngara kama Aliyewahi kuwa Mbunge kwa kipindi cha 2015-2020, Alex Gashaza na wengine kama Issa Hussein Samma, Dr. Sengati na wengine ambao wanapigiwa chapuo na wazee.

Yapo majina ya vijana pia akiwemo Mheshimiwa Mbunge wa Sasa Ndaisaba George Ruhoro anayetetea nafasi yake, Dotto Jasson Bahemu mwandishi na Mtangazaji wa Clouds Media Group, Hilal Alexander Ruhundwa ambaye alitia Nia Katika Uchaguzi Mkuu uliopita na wengine kundi hili linapiganiwa na Vijana. 

Kitakachotokea, ni Nguvu ya Ujana vs Wazee.

Wapenzi wa michezo wa masumbwi, usiku wa kuamkia Leo wameshuhudia mapambano japo UL kuwa wa Kiini macho!!!!  Ni kati ya Mike Iron Tyson na Jake Paul.

Kuna la kujifunza hapa…..

Jake Paul kijana mbichi kabisa, miaka 27 amemchapa kirahisi Mike Tyson katika pambano la uzito wa juu.

Mike Tyson mwenye Umri wa miaka 58 ambaye ni Bondia mstaafu,  alifanikiwa kurusha ngumi 18 pekee katika shindano hilo la dakika 16, ikilinganishwa na 78 kutoka kwa Jake Paul.

Je, WASTAAFU watafuta dafu mbele ya Vijana 2025?

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *