Jiji la Dar linakua kwa kasi kubwa huku walio wengi wakihisi ndio sehemu pekee rahisi kupata fursa, kwani sehemu zingine mikoani uwekezaji sio mkubwa na hali ya kipato ni shida, japo huko vijijini maisha ni rahisi kuliko Dar lakini kupata hiyo pesa ndio mtihani!
Wabongo wengi wakipata Elimu ya Secondary au Chuo, kuishi kijijini au kazi za Kilimo, ufugaji na uvuvi wanaona sio size yao, wanataka white collar jobs ambazo ni mjini!
Serikali imeshindwa kushawishi vivutio vya kuongeza kipato nje ya jiji ikiwamo kutoa Elimu ya kujitegemea zaidi ya Elimu inayomjenga mtu kuajiriwa!
Serikali itumie kutoa mikopo kwa vikundi vya vijana kulingana na Elimu zao ili kuanzisha biashara, kilimo, mifugo, uvuvi.

Train ya mtaani inayotumia umeme na kutumika kwenye bara bara moja na mabasi ya kawaida. Je kwa umeme wa Tanesco, mradi unaotegemea ueme tutauweza ama ni ndoto za mchana? Na kama yatapita kwenye mahandaki/shimoni, je mvua za el nino na ukosefu wa mitaro ya maji safi kwenye miji yetu mikubwa kama Dar hazitogeuza mcharuko wa kukimbia foleni na kuwa mkebe wa vifo kwa watumia train ya umeme? Pengine haya maswali yameshafikiriwa na kuona si kizuwizi cha kuboresha njia za usafiri Dar es salaam na TRC, shirika la reli Tanzania.
Dar imejaa na inaongezeka daily, hesabu abiria wanaoingia na kutoka dar kila siku ndio utaelewa!
Muonekano wa reli za umeme za masafa mafupi mjini ni kama hii: Gusa maandishi ya blue
Nimemsikia Mkurugenzi Mkuu TRC akisema Shirika lake lina mpango wa kujenga Reli Dar.
Ninashauri hizi njia za mwendokasi BRT ni utaalam wa kizamani, hizo njia badala ya kutumia Mabasi ya Mafuta, watumie Reli za umeme na kuweka mabehewa yenye kubeba abiria wengi zitakazokwenda kwa kasi zaidi na kuondoa hayo mabasi.
Sehemu zingine wanaweza kutumia underground trains, ambao ni mfumo wa kupitia kwenye mahandaki ya wazi ama yaliyofunikwa (shimoni) hususani sehemu zilizojengwa na kuwa na msongamano mkubwa.
Hali hiyo itapunguza foleni Dar es Salaam. Masaa yanayopotea kwenye foleni inadhoofisha uchumi.
Kila la kheri katika kuboresha miundombinu Dar.
Tanzania ni yetu sote!