UKIKUBALI KUPIGISHWA KWATA,UTAPIGA MPAKA UFE

By admin Mar 15, 2024
Wanafunzi, wafuasi, wasaidizi wote - basi tuikanyage hii ardhi kisawa sawa ili tuthibitishe kuwa sie bado ni vijana. Wale wazee kama kina Mugata waache wapumzike, mbio za uongozi ni zetu vijana. Si unaona tunakimbia kimbia tuu maswali, wajibu, ila bado tunaeleweka. Picha na Mwalimu Mjanja Mjanja.

Na: Mk Mjanja Mjanja

Mnamo wa saa za mchana, Wilayani Ngara vumbi lilionekana likitibuliwa, ardhi ikikanyagwa kwa kishindo na sauti ambazo hazijapangiliwa kiutalaam zikitoka kwenye koo za aina tofauti tofauti, shingo zenye urefu wa kila aina, za wavulana na madume ya kila umri – wazee kwa watoto. Yote haya yalitokea nikiwa na safisha shamba langu la migomba, usafishaji unaojulikana kama gusharila. Nikasema nisishangae tuu kwani hii ni fursa ya kipekee, kuinakili ili historia isije sahaulika nikaamua kujipepesa mfukoni kama nilikua na kalamu ama hata kifaa chochote. Nikakuta kalamu niliyokuwa nayo ilikua haiandiki tena ila kwa bahati nzuri kwenye koti langu nikakuta kamera. Nikasema na zoezi lote hili ambalo wanaume wenye vifua vipana, misuri na wengine wanavipara kabisa lazima litunzwe ili taifa la kesho lije kujua kuwa baba na ndugu zao nao walibeti, iwe kwa hiali ama kwa upendo. Tazama kwenye picha hapo juu jinsi wengine hata wamesahau kuomba sare zilizoporwa wakaamua wajiunge na mchaka mchaka ili kuamsha damu kwani mazowezi siku zote matunda yake ni mema kwa mwili wa binadamu.

Kwa kutumia Kamera ya Ngara TV, nilifanikiwa kunasa mchakamchaka uliobeba vioja vya wababa wa familia zao wakikimbizwa kama mgambo wabweni vile!

Bahati mbaya haikumnasa mwanadiplomasia wa vijijini ikabidi kumuuliza kwanini asiungane na bosi wake kuandamana? Alijibu hata akilala ndani tu posho yake lazima idondoke.

Sikiliza bhana, na sauti yake inayotokwa kwa tabu kama vile imeminywa puani, mimi sio wa level hizo. Acha hao mambo waandamane. Watampokea na watamaliza. Kwani umeniona mie napigishwa kweto na kujitoa muhanga kama hao wasiojua kesho mlo wao utatokea wapi? Mie ni mtu mzito kwani wanasiasa wengi vitu vyao haviendi mpaka wananipia mie. Unajua nafanya kazi na wanasiasa wangapi na hata kama upepo ukivuma vibaya, kwa level yangu nitadandia tuu sehemu. Mie sio kama hawa watoto wageni kwenye siasa ambapo wengine wanaburuzwa tuu bila hata kupewa mkataba wa kazi. Lazima wabembeleze tu ili maisha yasonge mbele.

Kwenye picha wameonekana watu wazima na familia zao wakikimbizwa mwisho wanaambulia 30-30 ambazo hata wine hazinunui.

Wameacha familia na kusafiri maili nyingi, na Mikoa kibao kuja kumtumikia mfalme wao; badae watalialia watoto wakiiga tabia zao? Ni aibu kwa kweli.

NGARA TV inataka kujua kwanini mwanadiplomasia wa kitaa haonekani kwa mikutano? Ama nauli na bajeti ilibana safari hii.

Sio lazima ila Maadam napata changu, na maisha yanaenda na migomba yangu inastawili vizuri tuu. Acha wao waandamane. Watetee bosi wao ambaye ameshindwa kuonyesha ripoti ya yale aliyoyafanya kwa muda aliotawala ila anaishia kuona wazee na wale waliomtangulia kama wachawi kwani safu yao angalau ilipanga vizuri mafanikio wa yale waliyoyafanya.

Kwenye picha wameonekana watu mbalimbali hata wasio na uniform, na katikati kuna wanafunzi au ni green guard au watoto wa Shule! Ila kwa kuwa hawa wasiokuwa na sare ilibidi wajitolee kuungana na msafara, ndio njia ya kubembelezwa ili waangaliwe kwa jicho la huruma kwani vifaa vya kazi wameporwa, na pengine hata sare walishaporwa kwani line up (idara) yao mara nyingi ingekua kwenye kunakiri kwa makini matukio ya habari na sio kutupiwa pembeni ya msafara mzima na kuchezeshwa ngoma kama watu wasiokuwa na thamani tena kwenye squad ya muheshimiwa mwenyewe. Anyways, kubembeleza ndio njia pekee itakayompatia 30-30 ya kuvuta jasho baada ya kukusanya vumbi na jasho la huu mchaka mchaka.

Kama ni wanafunzi, hayo ni makosa. Hao waachwe wasome sio kuambukizwa siasa uchara itakaowatesa miaka ya mbele. Watoto wa shule waacheni mashuleni, kama nikuwazawadia 30-30 wapeni tuu wapate hata soda bila kuwakatishia masomo, jameni.

Acha waisome hao makuruta feki tu.

Chama CCM mama wa TAIFA, angalia tabia za walimu kukimbilia Siasa na kutelekeza kazi ya kufundisha watoto. Huyo mfalme anataka kuua kizazi cha Ngara.

Kutoka migombani kwangu, nimeona ninakili hili tukio ili angalau lipeperushwe Ngara tv. Ngoja niendelee kushughulikia shamba langu kwani na amini kula kwa mikono yangu na sio kutegemea kujipendekeza kwa hao wanaoaminisha jamii ya kwamba ni imisole lakini wanaishia kushikishwa 30-30 kwa ushiriki wao wa mbio katika vumbi na jua kali kama inavyoonekana kwenye picha.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *