AIBU KWA MACHAWA, VIJANA WANAOTUMIKA KAMA KOLEO

By admin Mar 13, 2024
Aliyedai kuihama Chadema na kuhamia CCM huko Kabanga, Kagera Tanzania. Picha na SimamiaTV.Pichani, Wa pili kutoka kushoto, aliyevalia nguo zinazoonekana kama ni za mgambo (suruali na buti) na juu t-shirt inayooneana kama ni rangi za bendera ya Chadema akitambulishwa kwa umma kama mwana CCM mpya aliyehama chama cha Chadema. Wachambuzi wameulizia uhalisia wa ufuasi wa Chadema kwani hata Gwanda - vazi maarufu kwa wanachadema, halifanani na vazi la huyu mwana CCM Mpya aliyejitokeza huko Kabanga, mkoani Kagera. Picha na Simamia TV.

Jana ulimwengu ulishuhudia jinsi gani umasikini unavyotuendesha. Tunafanya lolote ilimradi tuwe karibu na watumishi wa serikali. Tunakubari kutumika kama kalai inayobebeshwa udongo na zege na kujisahau ujenzi ukiisha itatupwa tuu. Thamani yake inathaminika pale inapokua inahitajika. Vijana wa leo tumekomalia kuwa chawa ili mradi tuu siku isogee tuu.

Tunavyojishika kwenye jamii ni tofauti na maneno tunayosemezana. Vijana tunaonena donge na tunachukiana. Tukivaa sare za chama sote ni kijani ila moyoni kuna wengine ukijani umefifia na wapo nasi ilimradi tuu tusionekane mbuzi ndani ya kikundi cha kondoo. Hatufirii tunayoyatenda na tunayoyafanya.

Binafsi nimekerwa sana kuona mawazo huru kwenye makundi ya facebook na what app yanaminywa. Vijana tunatumia nguvu nyingi sana kupendezesha mtu kwa pambio na nyimbo wakati matendo yake yanakinzana na kile anachokisema mdomoni. Jitu ambalo linajijali lenyewe na kesho tuseme umechoshwa na hizi sifia sifia utajikuta unakua muhanga utakayekimbilia kwenye vyombo vya habari kama Simamiatv kwani wale huwa wananyosha hata pale palipopindishwa pindishwa kwa makusudi.

Sawa, wengine hamjapendezwa na ujumbe ulioandikwa na Sam Ruhuza. Ujumbe unaoihusu Wilaya ya Ngara, wilaya ambayo imekua fata fata upepo wa siasa zilizoleta umasikini mkubwa kuliko nguvu zinazotumika katika kuboresha maendeleo.

Yule mwanahakati mnayemuita kijitu, Baraka Bitariho ambaye haoni aibu kujiita Muyovu naye mmetoa kwenye magroup mbali mbali ila yeye kama yeye bado anafikisha ujumbe wake kwa wahusika. Tena anafikisha jumbe zake kwa style ya kiyovu ambayo inatumia lugha iliyopinda pinda na yenye mafumbo.

Hizi jumbe za kuamsha uelewa msizichukie. Vijana, hatujui kesho yetu itakuaje, hasa kwenye haya mazingira ya maigizo ambapo jitu lolote kutoka mtaani linapewa pesa kidogo na kuvaa jezi za Chadema na kujifanya kurudi CCM mbele ya umati wa watu. Huyo anayedai ni Chadema akiulizwa maswali kadhaa juu ya Chama Cha Demokrasia, hajui kwani yeye kwake safu ya uongozi iliyokua juu ndiyo Chadema kwake. Tukiwa tunadanganya, tufikirie na kutafakari.

Kabanga: Vijana, makada wa CCM wakiimba Kazi iendelee.

Vijana tunaonekana mburuta ambao hawana hata uwezo wa kudanganya kitu kikaonekana ni kweli. Kwa mwenendo wa kuunga unga, danganya danganya, kanusha taarifa ambazo zinaelezea maisha yetu nyumbani kwetu ili tuonekane ni wazalendo na chawa imara havitosaidia Ngara yetu.

Ninapokua kati kati yenu huwa nafatilizia tunachoelekezwa kufanya lakini moyoni naumia. Vijana, tusiendelee kuwa wajinga wa dizaini hii. Baadhi yetu tunadai tumesoma ila ndio tunashinda tukipanga jinsi gani ya kukomoa wenzetu. Mtu hujatumikia hiki chama kama sie tuliosota miaka nenda rudi ila kisa unajiita msomi unapewa posho kubwa na uwanja wa kujionyesha kwenye suti zako za kuazima. Unachodai ni usomi unautumia kufungua kesi zisizo na miguu wala mikono, unatumika kuteka majukumu na madaraka ya wasaidizi wa Mbunge, na unatumika kuuratibu upumbafu na ujinga ukiamini wewe ni msaidizi Bora! Kwahi huko Pwani ulipokua upepo ulikua unavuma sana ukapeperushiwa huku kwetu unapoona aibu hata kufikia nyumbani kwenu?

Unakumbuka kwamba wewe huyo unaemsaidia uliwahi kumchafua?

Umesahau ulivyokatwa makonde na akina Uncle D?

Umejisahaulisha kuombaomba ?

Chupa za Dompo haziwezi kukuacha salama. Labda uombe radhi kwa Mzee Charles.

Kumpigia baba! Umewahi kuona wapi?

Imeandikwa, waheshimu Baba na Mama upate miaka mingi na Heri Duniani. Wewe Mamlaka unapata wapi?

Sawa vijana mmefanya mengi nata kutoa wengi kwenye magroup yenu na kubeza jumbe zenye manufaa kwa Wilaya ya Ngara.

Kwa haya matendo yenu yanawaonyesha kwa jamii kama mna matatizo wa afya ya akili. Watanzania wengi wanawaona kama Ikisamunjojo(Kobe). Ipo siku mtakimbiana na kulilia kwenye vyombo vya habari kuwa siasa ni mchezo mchafu. Ipo siku mtajikuta mnajipendekeza kwa mshindi na viongozi wapya.

Tutambue kuwa sie bado ni vijana na bado tunamaisha marefu hapo mbeleni. Tuheshimu wale waliotutawala na wanaotuwala. Kutukana wazee, kuwabeza ama hata kuwatwanga makonde sio sifa zitakazotuletea matunda mema. Wananchi hawaongei ila wanatazama na kusikitishwa na maigizo yanayoendelea. Pengine tusifurahie kuimba miaka mitano tena bali tujiulize ni kipi tulichokipanda na kukivuna ambacho watoto na ndugu zetu watanufaika nacho? Kama wazazi wetu wenyewe wanajuta kutumia nguvu na pesa zao kutupereka shuleni, je tunayoyaahidi na kujitamba ni zao la kufika Bungeni, kuishi kwenye majiji makubwa na kuwazawadia wazazi wetu na ugomvi unaoshusha hadhi zao kwenye miji yao; miji ambao wao ni wafalme kwani ndio wanafanya maamuzi yote. Miji ambayo wakazi wa utawala wao walitengeneza mazingira mazuri ambayo ndio yamekuelimisha na kukuza mpaka kufikia hapo ulipo. Tuombe Mungu atupunguzie haya madhara ya afya ya akili kwani hii mienendo yetu mibovu inavunja na si uimarisha Ngara Yetu.

Aliyedai kuihama Chadema na kuhamia CCM huko Kabanga, Kagera Tanzania. Picha na SimamiaTV.

Kama Ndugu zako wanakuona kituko, wazazi wako ama wale waliotawala kabla yako wanajiuliza kama wanachokiona na kukisikia ni zao la kusoma na sio kuelimika, kama hata kupumzika hurudi jimboni ama nyumbani kwani unakuona hakufai na unaishia kupumzikia huko unapopajua, iwe lodge ama nyumba yako ya pili, iweje wewe ujiamini kuwa na hadhi ya kunyamazisha wengine kwa kubeza ama kuwatoa kwenye magroup? Unadhani kulisha wenzio maoni na mawazo yako ndio unawatendea haki ama ndio unatimiza nia ya kuwadidimiza na kuuwa jamii unayoijaribu kujenga?

Msomaji, wewe unajitambua na usikubali ufungiwe kwenye jamii ambayo inatamani iwe na maoni ya upande mmoja tuu. Maigizo mengine unayoshuhudia yanasababishwa na changamoto za afya ya akili ambazo zinakumba vijana wa kizazi hiki. Baadala ya kubuni njia za kujiunua kiuchumi wanaishia kuwa chawa tuu.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *