Kuliwahi kuwa na malumbano ya baadhi ya wanasiasa na viongozi kuhusu Bodaboda kuwa ni kazi au lah!
Nakumbuka, malumbano yalichukua takribani siku kadhaa; baadhi wakiitetea kuwa ni kazi inayowaingizia kipato vijana huku wengine wakiita laana.
Wengine walienda mbali wakauita ubodaboda kama kazi ambayo ni kichaka cha baadhi ya makundi ya wahalifu kwani huhusika na kusafirisha wahalifu, na wakati mwingine baadhi ya waendesha bodaboda wenyewe kushiriki katika kufanya uhalifu.
Wapo baadhi ya bodaboda waliofanikiwa kupata maendeleo kupitia kazi hiyo na kuweza kujenga nyumba, kuanzisha Miradi na hata kusomesha watoto shule za maana.
Lawama za bodaboda kwa jamii ni pale wanapohusishwa na mambo yanayohatarisha usalama wa raia kama vile kusafirisha wezi, kubeba wasichana wa shule au kujihusisha na mapenzi kwa wanafunzi na hata wake za watu.
Hivi karibuni, imebainika mchezo wa kisiasa ambao unawanasa bodaboda wa Wilaya ya Ngara katika harakati za baadhi ya Wanasiasa.
Mbunge wa Jimbo la Ngara George Ndaisaba Ruhoro ni mmoja wa watu wanaowaingiza bodaboda kwenye mtego huo kwa kuwatumia kupata Umaarufu.
“Mara nyingi sana anawatumia watu wake kutuita kama ana mikutano” alisema bodaboda mmoja aliyejulika kwa jina la Rama.
Mwingine aliyezungumza bila kutajwa jina lake, alisema “Sasa kama anatuwekea mafuta, na akatupiga posho ya elfu 10 kwanini tusimsinfikize?”
Imebainika kuwa Mbunge huyo wa Ngara, kupitia kwa mratibu wa shughuli zake na wapambe wengine humpangia ratiba za mikutano kwa kumpatia bajeti inayohusisha mafuta na posho za bodaboda ambao hupamba misafara yake kwa maandamano.
Aidha, hali hiyo pia inatoa fursa za upigaji kwa baadhi ya waratibu ambao hupata viwango wanavyotakiwa kulipwa Bodaboda na kuwapa malipo pungufu.
“Siamini kama tunacholipwa ndicho kinatoka kwa Mheshimiwa, kwasababu hatujawahi kuzidishiwa Lita 2 labda siku moja-moja huku Rulenge ndio anatoa mpaka elfu 10.” Alisema bodaboda alliefahamika kama Sinzo.
Kwa ushuhuda wa bodaboda hao wakizungumzia mikutano ya Mbunge ni kweli wanatumika.
Ushauri wetu, wasikatae kufanya kazi zinazowaingizia kipato. Ila, wachukue tahadhali. Wakumbuke Wanasiasa wanakuja na kuondoka. Muda wao ukiisha, hawatawakumbuka.