Mmoja wa wasaidizi wa Mbunge wa Ngara, Ndaisaba Ruhoro, ambaye anapenda sifa ama kwa kujua au kutojua kuwa anamchafulia njia boss wake ametishia uhai wa wandishi wa Habari wa Simamia TV.
Alitoa Kauli ya kuwateka, huenda ndio kazi yake! Alitoa Kauli za majigambo kwamba wao ndio wanaotembea usiku, wanaweza kufanya lolote na kwa muda wowote!
Msaidizi huyo licha ya kuwa ni tabia zake za misifa na kujigamba, alihoji kwanini Simamia Media haifiki kwenye matukio ya Mbunge licha ya kupewa majibu mazuri kuwa Simamia hajawahi kualikwa ikagoma. Kauli zake Bado zimetia mashaka.
Ikiwa ni siku Moja pia baada ya Moja ya taarifa iliyorushwa kuhusu Binti wa familia ya Kagaigai kukanusha taarifa za kusomeshwa na Mbunge Ruhoro, msaidizi wa Mbunge na wenzake wakaituhumu pia Simamia Media Group kwamba inatumiwa Kisiasa
Imekuwa kawaida kwa baadhi ya WASAIDIZI na wapambe wa Ruhoro kutumbua mitaani, kutoa maneno ya kashfa na hata kufanya fujo mitaanai
Vijana hao wakiwemo walimu, mlinzi wake na Wandishi wa Chombo chake wamezidi
Nyie bwana! Mbunge ana Pesa nyingi. Njooni tufanye kazi, anaweza akafanya lolote. Anaweza kumununua mtu yeyote awe mwanaume au mwanamke.