Ngara: Kero ya Barabara yawaibua wananchi wa Nyamagoma

By Titho Philemon Aug 17, 2024

Ikiwa ni mwezi mmoja toka ukarabati wa Barabara ya Mulonzi – Mkalinzi usimame kwa ubovu wa Trekta wananchi wa maeneo hayo wamekuwa na maoni tofauti kwa kile wanachodai kuwa msimu wa mvua tukianza ukarabati utakuwa na madhara kwa wananchi kwakuwa barabara haitapitika tena kwasababu ya tope.

Kwa upande wa wananchi wa Mukitoma, Kijiji cha Murubanga Kata ya Nyamagoma mahali ambapo Trekta hiyo imekwama kwa mwezi mzima sasa wamemuomba Meneja wa TARURA wilaya ya Ngara kuhakikisha anawasaidia kero yao hiyo ya barabara ili wanapoelekea msimu wa kilimo na mvua nyingi usafiri uwe wa uhakika na barabara ziwe za kupitika.

Barabara ya Mulonzi (Nyamagoma) hadi Mkalinzi (MUGANZA) ni barabara ambayo imekuwa ikitumiwa na wananchi wa kata hizo mbili katika Shughuli za Uzalishaji Mali ikiwemo Kilimo na Biashara hali ambayo kwasasa inawatia wasiwasi kutokana na mkwamo wa matengenezo hayo. Barabara hiyo ina Kilometa 17 ambayo kwasasa imekamilika kwa Kilometa 5 tu.

Wananchi wanasema endapo barabara hiyo itakamilika changamoto ya usafirishaji itakuwa imepatiwa Mwarobaini na maendeleo ya Kata hizo (Nyamagoma na MUGANZA) yatakuwa yamefunguka na kupelekea maendeleo na uchumi wa wananchi hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *