Akiongea na mamia ya washiriki wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la 14 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania (TET) iliyofanyika Ijumaa ya Disemba 6, 2024 jijini Arusha, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa amekemea tabia ya baadhi ya Wakurugenzi wa halmashauri wenye tabia ya kuweka vizuizi barabarani wakilenga kusimamisha maroli kutoka kwenye halmashauri zao bila kufuata utaratibu. Aidha, Waziri Mkuu amewataka Wakurugenzi wa halmashauri kuziacha barabara ili zitumike zinavyopaswa na kuongeza kuwa wenye kibali cha kuzuia barabara ni Jeshi la Polisi peke yake kwa ajili ya ukaguzi wa usalama.