WEZI WA NGARA FARMERS WAKAMATWE HARAKA

By Na Mwandishi May 22, 2026

Mkuu wa Wilaya ya Ngara ameagiza vyombo vya Usalama kufuatilia Wizi unaofanywa na baadhi ya watumishi kwenye Vyama vya Ushirika ili kuepusha hasara kwa Wakulima wanaotegemea vyama hivyo kuendesha maisha yao.

Kauli ya mkuu huyo wa Wilaya Kanali Mathias Julius Kahabi,imetolewa wakati wa ugunguzi wa chala kipya cha msingi cha Rulenge AMCOS Limited.

Akitoa salamu za Wilaya wakati wa ufunguzi wa AMCOS hiyo ulioambata na zoezi la kukabidhiwa Cheti cha Usajili, Kanali Kahabi ameeleza kuchukizwa na vitendo vya Wizi unaofanywa na baadhi ya watumishi katika Vyama vya msingi.”Wezi wamejaa Ngara Farmers, Ngara Farmers imeibiwa sana! Juzi juzi tu wamesimamishwa Meneja na Mhasibu” DC Kahabi.

Kutokana na hali hiyo, ameagiza vyombo vya usalama hasa Mkuu wa Jeshi la Polis Wilaya ya Ngara,na Mkuu wa TAKUKURU kuhakikisha wanafanya uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa.

Aidha amewataka Mrajisi wa vyama vya ushirika na Afisa Ushirika kushirikiana kukagua na kuwabaini watu wemye nia ya kukwamisha maendeleo ya Ushirika.

“Hivi vyama tunavianzisha kusaidia Wananchi tusiwakatishe tamaa” amesema.Tunatakiwa kuwa makini na kushughulikia haya mambo haraka, kuna mambo yanafanyika as if tuna buy buy time ili wezi watokomee kimoja,yaani hatuoni proper measures!