DOTTO JASSON BAHEMU ASHIRIKI MAZISHI YA MWENYEKITI WA CCM KATA YA NYAKISASA

By Na Mwandishi Jul 22, 2026

Na Juventus Juvenary – Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Ngara.

Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mheshimiwa Dotto Jasson Bahemu, ameshiriki mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Nyakisasa, Marehemu Zacharia Minani Mwanda.

Mazishi hayo yamefanyika leo Jumatano, Julai 22, 2026, nyumbani kwa marehemu katika Kijiji cha Kashinga, Kata ya Nyakisasa.

Akitoa salamu za rambirambi, Mheshimiwa Bahemu amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Marehemu Zacharia Mwanda, akimtaja kuwa kiongozi mwadilifu na mtumishi wa chama aliyetoa mchango mkubwa kwa zaidi ya miaka 20.

“Nimesikitishwa na kifo cha Mwenyekiti wetu. Nilifahamiana naye kwa muda mrefu na tulifanya kazi pamoja, ikiwemo wakati wa kampeni na hata nilipozuru kata hii mwezi Januari mwaka huu,” amesema Bahemu.

Katika kuendelea kuifariji familia, Mheshimiwa Dotto Bahemu ameahidi kugharamia masomo ya watoto wawili wa marehemu, mmoja wa shule ya msingi na mwingine wa sekondari.

Marehemu Zacharia Minani Mwanda alizaliwa mwaka 1963 na amefariki dunia mwaka 2026.