
Mbunge wa Jimbo la Ngara Dotto Jasson Bahemu amefanya ziara katika kata ya Kabanga leo Jumamosi Julai 25,2026.
Ziara hiyo inafuatia malalamiko ya baadhu ya Wananchi wa Kata hiyo kuhusu changamoto ya Upatikanaji wa maji.
Katika ziara hiyo Mheshimiwa Mbunge ameambatana na Diwani wa Kabanga Hafidh Abdallah,Mhandisi wa Maji Wilaya ya Ngara Simon Ndyamukama, Afisa mtendaji wa Kata hiyo Elian Bugoke na baadhi ya Wananchi, wakiwemo viongozi wa Junuiya ya watumiaji Maji.







