Kagaigai Ndani ya Ngara

By admin Dec 23, 2024
Kagaigai ni jiwe imara, umunyasiri ambaye hayupo tayari kupigwa teke na mambo ya leo, mambo ya kisasa. Naye anakiu kuona maendeleo sio story za mdomoni tuu bali maendeleo yananufaisha kila wana Ngara, wanawake, watoto, vijana, wanaojiweza na wasiojiweza. Anguruma eti wana Ngara wamechezewa sana, kudanganya sana tena na watu wanaokusa ujasiri wa kuonyesha wake zao hadharani. Aahadi Ngara yenye usawa na kujari hata wale wasiojiza. Anguruma makanisani, misibani, na hata kwenye kusanyingiko mbali mbali Wilayani Ngara.Kagaigai atinga Kanisani kumshukuru Muumba kwa yote na apiga hodi Ngara kwa style ya kipekee.

Mechi imeanza, harufu ya krimasi haifichiki. Wilayani Ngara, wanaodai kuwa na asilia ya Ngara warudi nyumbani gusangira tonge lililopo kabla ya mwaka kukatika. Wanavyoendelea kumiminika Asiliani, wanarudi na sura mpya na ujio wa hawa wanyamahanga wanapokuita kwao, hakika Ngara inapendeza kwani hodi hodi za kiuhakika hukusanya watu, kamera mbali mbali, tabasamu, na hata zile changamoto zinasauhaulika kwa muda. Kwa muonekano wa haraka haraka, ingekua vizuri kila siku wilayani Ngara iwe kama ni mwisho wa mwaka kwani hata kero zingeogopa kughathaibisha wana Ngara.

Kwa wana Ngara, Wanyamahanga ni watu wakuja ingawa tafsiri kwa wengine inaweza kutofautiana. Ila kwa wanangara wengine, tafsiri ya neno wanyamahanga ni kwamba wale wasiokuwa na asili ya Ngara. Sasa mgongano wa tafsiri na uelewa huwa si kitu kinachosumbua watu wengi hasa kama hata hawauoni wala kuelewa. 

Kwa andiko la leo, wanaokuja watatukimbia baada ya kuharibu koo zetu kwa manukato na kutulingishia magari na utajiri ambao pengine ni wakuazima.Wengi wao benki zikiwadai, watakimbilia kwenye media ili wavune huruma kutoka kwa wananchi na pengine kwa Raisi. Kama mkazi wa Ngara, nashukuru watembezi kwa kuipendezesha na kwa vihela ambapo tumepata fursa ya kutapakanya harufu za vyakula mbali mbali, mikaango ambayo inajumuisha ndugu na jamii na wengine hutuletea miondoko ya kipekee.

Wikiendi chache ziliyopita kupitia Simamia.com na Simamiatv, pale Nkundusi na katika mikusanyiko mbali mbali kanisani, mheshimiwa Steven Kagaigai alitushitukiza na ujio wake. Kwa miondoko yake tuu, mheshimiwa Kagaigai ni umunyamahanga asiyetaka kupigwa teke na asili ya Ngara. Huyu umunyasili, alitinga makanisani na staili fulani ambazo hatujazowea kuziona hapa Ngara wala kuziona muda wa Krismasi ama kwenye dakika kumi na nane za kuaga mwaka zinapokaribia. 

Kwa  kishindo kikubwa, mheshimiwa Kagaigai alitutambulisha  jiko lake, mpufa wake wa kumi na nne, mama mpendwa, mama aliyemtambulisha kama mke wangu ambaye ni mwalimu bila hata kutaja jina lake. Kwa waliokuwa wanasikiliza na kukodoa macho, basi waliamua kumuita aliyetambulishwa, Mama Kagaigai. 

Mama Kagaigai Akitambulishwa kwa wana Ngara na mchango wake usiofichika kama mwana mama na nguzo muhimu kwa familia yake na kwa mafanikio ya mumewe.

Akiwa na mama Kagaigai mbele ya umati wa watu, mheshimiwa Kagaigai alituonya tuogope wale ambao wanajitutumua bila kuwa na kifua ama uwezo wa kuonyesha mke/wake zao. Biblia inasema kila mwanaume anayependeza, ujue nyuma yake amesaidiwa na mwanamke. Kulingana na alichokisema Mheshimiwa Kagaigai, mchango wa wanawake sio wa kupuuzia kwani hata hao wanaodai kuwa na nguvu na uwezo wa kuona kama kuna binadamu wasiofaa, wasidanganye jamii kuwa wanaweza kuwa kamili bila kuwa na mwanamke.

Na kama huna mwanamke, ni maendeleo gani utakayoyaleta kama hata unaficha mafanikio uliyomletea mama yako, dada yako ama yule anayekuandalia nguo unazovaa ama kukutunzia watoto?

Mheshimiwa Kagaigai alisema mengi na hata alidontosha noti za kutosha hasa kwa ajiri ya kwaya na miradi inayosaidia wasiojiweza. Kwenye maongezi mengi, alisisitiza uwezo wa kujari wale ambao pengine wamesahaulika na jamii kama wale wasiojiweza. 

Siwezi kujitamba peke yangu, mfupa wangu na nguzo muhimu kwangu ni Mama na mtu asikudanganye, wanawake wana mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa letu.

Kwa mchango na maneno yake, mheshimiwa Kagaigai ni mtu wa watu anayejari familia. Ni umwasili, umungara ambaye anatakia mema Ngara Yake. Kutokana na miundo mibovu ya kimawasiliano, Ngaratv haikufanikiwa kupata mheshimiwa Kagaigai kwa njia za simu ili atoe mchango wake kwa andiko hili. 

Tunaamini tutajifunza mengi kutoka wenye mdahalo utakaofanyika Kabanga tarehe 26, December, 2024. Mdahalo wa maendeleo umeandaliwa na Simamia Media Group na utarushwa moja kwa moja kupita youtube na social media nyingine ili wale walioikimbia Ngara waweza kufatilia kinachoendelea. Tutegemee Kamera Nene na wasaidizi wake wasije kutuangusha kwani kazi zao zinaleta maswala ya Ngara ulimwenguni kwa kazi zao za kimedia. 

Kwa wana Ngara, tukaeni mkao wa kula ili tuone kila anayeingia atakuja na mke wake ama kama zile nguvu za ujana zita aminisha jamii kuwa wenza wao wapo ngangari kusukuma gurudumu la maendeleo ambayo ni muhimu ili kuipata Ngara yenye nuru na maendeleo. 

Mdahalo na shughuli zote tuzifanyazo ni kutokana na uwepo, ukarimu, na michango yenu. Tutakua hatutendi haki kutotambua michango yenu ya kimawazo, kiushirikiano, na kifedha. Ngara njem itapatikana kwa kushirikiana na kupora fito huku tukijenga nyumba ile ile itaturudisha nyuma kuliko kuungana na kuipendezesha na kuimarisha nyumba yetu ambayo sote tunaiita Wilaya ya Ngara.
Moja mambo mazuri ambayo kigogo mzito ambaye ni katibu mkuu wa Television ya Taifa (TBC) ni kujikoa kwa hali na mali katika kusaidia watoto wasiojiwezaa. Si tuu kupitia makanisani bali hata hapa mji mdogo wa Rulenge, bwana Kagaigai ametoa mchango wa vyakula na ukarabati wa jiko katika hifadhi ya watoto ambao kwa namna moja ama nyingine hawajiwezi. Kule Makanisani ametoa michango kuwezesha kwanya kutoa albamu, na uwepo wake ndani ya Wilaya ya Ngara amekua akionekana katika misiba na shughuli mbali mbali za kijamii. Pia ni mmoja wa wanangara ambao si wakazi wa wilaya ya Ngara kwani matakwa ya kazi zake hayawezi kutimizwa akiwa Wilayani Ngara. Gari lake ni moja ya chuma kinachopendezesha Ngara msimu huu wa sikukuu na haki ya Mungu hali iliyopo ingekua ni hali halisi ya maisha ya mwana Ngara, pengine hizi changamoto zingebebwa kijamii na kutokua mzigo kwa michango ya wachache. Pia shukurani ni kwa wale wanaojitoa kwa hali na mali kuhakikisha wasiojiweza wanapatiwa haki za kimsingi na mengine yaendelea. Na mwandishi wenu: Vyihoze.

Kama timu Ngaratv, wakazi wa Ngara, tunakukaribisha baba yetu, kiongozi wetu na pengine kama andiko lilivyoelezea mwanzoni, karibu kama Mnyamahanga asiyekuwa tayari kupigwa teke na asili zetu ama kasi za maendeleo ambazo zipo Wilayani Ngara.

Krimasi njema, na Mwaka muumalize salama. Kamera Nene mulika bila kukonyeza kila style na kila neno litakaloongelewa katika mdahalo. Na mwandishi wenu Vyihoze.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *