C.d.e Herbert J. Muhile atangaza nia ya Ubunge Jimbo la Ngara, 2025

By Titho Philemon May 10, 2025
C..d.e Herbert J. Muhile mtia nia Ubunge Jimbo la Ngara

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani nchini Tanzania, ndani ya Jimbo la Ngara ongezeko la vijana katika kuwania nafasi ya ubunge limezidi kuamsha sura na taaswira mpy na tofauti kisiasa. Hali hii imeonekana kudhihirisha utayari wa vijana na wazalendo wa kweli wa Ngara kutaka Mageuzi ya Kisekta ndani ya jimbo la Ngara kwa manufaa ya wanangara. Hakika Vijana wameamua!

C.d.e Herbert Muhile ametangaza kutia nia nafasi ya ubunge kwa Jimbo la Ngara kwa Tiketi ya CCM huku akiweka wazi kuwa anao uwezo, ukomavu, uzoefu, hekima, busara, maarifa, na ubunifu wa kushika nafasi ya Mbunge wa Jimbo la Ngara.

Aidha C.d.e Herbert Muhile amesema anaomba nafasi hiyo akiwa anaelewa kiu ya wanangara kupata aina mpya ya uongozi wa zama za sasa na za kileo utakaotoa matumaini mapya katika kuijenga Ngara Mpya.

Ujio wa C.d.e Herbert Muhile kwenye kinyang’anyiro cha ubunge wa jimbo la Ngara kunaongeza idadi ya wagombea pamoja na ushindani ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ngara. Ikumbukwe kuwa, Comrade Muhile amekuwa kada wa CCM kwa miaka mingi sasa toka akiwa mdogo pamoja na kushirikiana na watia nia wa ubunge wa Jimbo la Ngara kwa miaka ya nyuma hali inayomuongezea uzoefu wa kimazingira kwa maeneo mengi ya Ngara.

Endelea kutufuatilia Ngaratv.com kwa taarifa zaidi..!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *