Kutokana na yale yanayoendelea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji ni uonevu Kwa Vyama vya upinzani Nchini.
Tunafahamu Tarehe 27 November 2024 kutafanyika uchaguzi wa kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa/Vijiji na vitongoji.
Kinachoendelea Kwa Sasa ni katakata ya wagombea wa Vyama vya upinzani Huku wale wa Chama Tawala wakiendelea kunywa Supu Kwa mlija jambo Ambalo linaleta picha mbaya Kwa jamii yetu hata ya kimataifa.
Tume ya Uchaguzi lazima ibebeshwe lawama zote Hizi maana wao ndio wasimamizi wakuu wa hili,Kuna wagombea wa Chama A wamepitishwa baada ya kuandika kazi yao ni Ujasiliamali Huku wa Chama B akiandika hivyo anakatwa na kuambiwa HIYO kazi haipo,Sasa maswali ni mengi kwanini mmoja akatwe na mwingine aachwe?.
Ushauri Kwa wahusika wawaache wagombea wote wapite na wananchi ndio wawe waamuzi wa mwisho Ili kuchagua viongozi wawatakao.
Pili Tuepushe chuki Kwa viongozi watakaopita bila kupingwa maana Hawa viongozi ndio wanaishi nao huko chini na sio vyema kuwatengenezea matatizo ya wazi na pia kuepusha lawama zisiszo na msingi.
Mwisho Kabisa Kuna haja kuwa na tume huru ya Uchaguzi ambayo haisimamiwi na Serikali maana Serikali inatokana na chama kilichopo Madarakani na ndio inachagua hawa wanaosimamia tume hivyo maswali kuwa mengi kuliko majibu katika utendaji wake.