KATIKA HILI LA HUJUMA, ninaomba Mbunge wetu wa Wananchi wa Ngara Hon. Ruhoro nimpumzishe kwa Muda (Hahusiki).
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kwa maana ya Utawala na Kamati zake zote kumejaa uozo!
Kutokana na uozo pamoja na figusi za hapa na pale zizazoikabili Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mipango mingi ya kijamii imekuwa haitekelezeki na kufuatiliwa! Sekta ya kilimo, sekta ya viwanda na Biashara, sekta ya Utawala, sekta ya Madini, sekta ya miundombinu, Sekta ya Afya, Sekta ya Uhamiaji na sekta nyinginezo.
Halmashauri ya Wilaya imekuwa ni Halmashauri maalumu kwa watawala (wageni) kuja kuchuma kile kilichopo na kisha kutokomea. Katika KUTEKELEZA uchumaji Mali huo kwenye Halmashauri ya Ngara, hao watawala wetu wasio waadilifu (wageni) wamekuwa na kasumba ya kuanza kujenga utimu yaani makundi na kuigawa Halmashauri yetu na kuwawekea vikwazo Madiwani na Wanaharakati wote ambao wanakuwa wakionyesha kutopendezwa na mwenendo mzima wa Halmashauri hali ambayo inaumiza na kusikitisha sana.
Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ngara imekuwa ikiripotiwa kufanya mambo mengi ya SIRINI ikiwemo kutaka kutumia Tsh 100,000,000/= yaani Shilingi za Kitanzania Milioni Mia Moja KUTEKELEZA marekebisho ya magari hela ambayo ingeelekezwa kwenye Miradi ya Umma ingeweza kutupatia matokeo ya dhati na kuistawisha Halmashauri Yetu.
Ninaomba kuishauri Ofisi ya DC – NGARA kuhakikisha inapanga vipaumbele vyake vya ziada nje ya bajeti ya Halmashauri, yaani Rehabilitation Allowances Analysis kwenye magari ya Halmashauri pamoja na starehe zote ifanyike baada ya kuwa wamejiridhisha kwamba FUNGU LILILOPO na lililotengwa kuiendesha Halmashauri linakidhi walau 70% ya ukamilifu wa bajeti ya Halmashauri kwa mwaka husika, nikiwa na maana kwamba Bajeti ya Halmashauri iwe Social Based Budget (SBB) na siyo Administrative Based Budget (ABB) hapo tutafika. Tusipolizingatia hilo Ofisi ya DC itaanza kuchukiwa na wana UCHUMI pamoja na wadau wa Maendeleo Ngara kutokana na hizo Consistent Leaking Informations ambazo zinadhihirisha udhaifu wa kiutendaji.
Kwa upande wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara (DED) Ndugu Solomon O. Kimilike tatizo la mfumo wa utendaji na uwazi katika utendaji limekuwa sugu!
Madiwani wamepungukiwa Thinking Capacity kutokana na mfumo wa maisha mliowajengea, kiasi cha kushindwa kupigania maslahi mapana ya wanangara na kuanza kupigania maslahi binafsi yasiyo na tija kwa Wanangara.
Kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Ngara yapo mazuri ya kupongezwa ambayo hata kwa macho mtu anaweza akayaona, lakini zile hujuma bubu ambazo mnafanyiana ninyi kwa nyinyi ndani ya Baraza la Madiwani nazo tuna taarifa zake.
Stendi ya Ngara Mjini imekuwa CHAFU, Soko la Ngara Mjini ni CHAFU na mpangilio wake ni mbovu wakati Kodi mnakusanya kila kukicha, ila mapambano yenu yanabakia Fulani asiwe Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, Fulani asipewe Connection hii badala ya kurekebisha Miundombinu yetu. Je Posho zetu wananchi mnakula za nini huko katika Halmashauri yetu ?
Mkurugenzi kama Msimamizi Mkuu wa fedha za serikali katika Halmashauri anapaswa kuhakikisha anasimamia kikamilifu matumizi ya pesa za umma pamoja na zile za Halmashauri katika Miradi yote kwa kushirikiana na Madiwani badala ya kushirikiana kuihujumu Ngara!
Imefika Hatua Ngara kwa sasa Mbunge wa Ngara Hon. Ruhoro akitetea Kitu Bungeni chenye maslahi ya watu, ndani ya Halmashauri (Magenge) ya watawala yanaungana kutia Dosari hoja nzuri zenye kuishikamanisha jamii zinazotolewa na Mbunge wetu.
Ninazidi kujipa muda zaidi kuifuatilia Ofisi ya Mkurugenzi ili nijue ni kwa namna gani ameshikamana na wapiga MADILI kuihujumu Ngara na Wanangara wote.
Nayaongea haya kama Kiongozi Mkuu wa Vijana wa CHADEMA ndani ya wilaya ya Ngara mwenye jukumu na mamlaka ya Ku-oversee hali zote zinazoweza kutia doa wilaya yetu.
Leo nimeangazia hizi ofisi mbili ya DC na DED kama ofisi Mama ndani ya Halmashauri.
Kwa Waraka huu, naomba TARURA, TANROAD, TANESCO, RUWASA pamoja na Idara ya Afya mjiandae kupokea ujumbe wenu pia.
Ngara bila Hujuma inawezekana sana. TUSIPOSHIKAMANA pamoja mambo yataharibika sana.
Madiwani punguzeni woga. Hao watawala wa kupita watawapotezea sifa huku mtaani.
Nina TAARIFA kuwa kuna wafanyabiashara wa Ngara ambao wanashirikiana na Halmashauri katika kuingia kandarasi mbalimbali na kuwa under qualify wengineo kwenye huo mfumo wao mpya uitwao NEST.
NGARA IMEJAA UOZO!
KWALEO ninaomba niishie hapa!
NB:- KWA KIONGOZI au Mtawala wa Ngara atakayehisi nilichokiandika hapa hakina maslahi mapana na wanangara au pengine hakina ushahidi nitawapatia taarifa za kina kuhusu kila hujuma niliyoianisha humu!
DED NGARA, na DC NGARA hongereni kwa kazi nzuri lakini rekebisheni makandokando yote ambayo mnahisi hayako sawa katika ofisi zenu. Soon nitakuja na lingine zito endapo hamtatafakari haya kwa umuhimu.
Asante ⚖️🙏🙏🙏