UVCCM bila BAVICHA ni sawa na GAZETI bila Mhariri

By Titho Philemon Aug 13, 2024

Pichani ni Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa MWL. JOHN JUSTINE PAMBALU (Kushoto) akiwa pamoja na Ndugu TITHO DYAKIYE PHILEMON (kulia).

Tunatafakari namna bora ya kuwakomboa vijana wa Ngara ambao:-

  1. 70% ya vijana wote hawana VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA) na 30% ni wale wanaozipata kwa sababu za kitaaluma.
  2. Zaidi ya 65% wanaamini kuwa mpinzani ni kuruhusu kubambikiziwa kesi za uraia.
  3. 85% wanaamini balozi wa CCM ndiye mwenye sifa ya kunyenyekewa na kutoza faini.
  4. 93% wanaoamini kwamba ni sahihi ofisi ya Kijiji kumfunga mtu siku tatu kisa tu kashindwa kutoa Rushwa kumaliza kesi inayomkabili.
  5. Zaidi ya 60% wanaoamini kwamba CCM ndo serikali na KATIBU WA CCM wa kata anaweza akamuamrisha VEO au WEO kuamua kinyume na sheria kwenye haki za wananchi.
  6. Zaidi ya 70% wanaamini kuwa usipokuwa CCM huwezi kuajiriwa na serikali.
  7. Miili yao iko chini ya mamlaka ya POLICE na MIGAMBO

UVCCM bila BAVICHA, ni sawa na GAZETI bila MHARIRI.

Karibuni sana BAVICHA📍

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *