Jimbo la Ngara bila Ndaisaba George Ruhoro tungekuwa mbali sana Kimaendeleo

By Titho Philemon Aug 10, 2024

KWA MUJIBU wa Ibara ya 8 (1)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali
itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi.

Kwahiyo, kila kiongozi aliyechaguliwa na wananchi haombwi kuwatumikia wananchi bali ni wajibu wake wa msingi katika kuhakikisha wapiga kura wake (wananchi) anawatumikia na wao kujenga imani njema dhidi yake.

Mbunge wa Jimbo la Ngara Ndugu NDAISABA GEORGE RUHORO amekuwa ni Mbunge ambaye toka aanze kuitawala Ngara:-

  1. Hajawahi kuibua mradi wowote wa kwake binafsi na akaupa nguvu katika KUFIKIA mafanikio na hatimaye kuinufaisha jamii ya Ngara. AMEKUWA ni Mbunge ambaye ni MTU wa dhihaka hususani dhidi ya mifumo ya wabunge waliomtangulia pasipo kuheshimu JITIHADA zao.
  2. Hajawahi kuchochea ueledi wa kiutendaji kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ili kuweza kumaliza kero ambazo zingetakiwa kushughulikiwa na mamlaka za Halmashauri. Kwa maana nyepesi, tungekuwa na Mbunge makini haya Mambo yangekuwa yameshafanyika mapema sana na kuineemesha jamii.
  3. Hajawahi kuhamasisha maendeleo binafsi kwenye serikali za mitaa na vijiji ndani ya Ngara tofauti na kutangaza vipaumbele vilivyomo kwenye bajeti ya Serikali na kusimamia kile serikali ilichokielekeza maeneo husika. Katika hili ninaweza kusema washukuriwe wabunge waliomtangulia pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kwa sasa – uchapakazi wao na hamasa RUHORO anapaswa kujifunza sana. Mheshimiwa GASAHAZA alitengeneza njia pasipokuwa na njia Kitongoji cha Bitunga Kijiji cha Mkalinzi ndani ya kata ya MUGANZA (Ngara) akahamasisha ujenzi wa Shule mpya ya msingi, akateseka field kulisimamia hilo. Wananchi wakaamua wamzawadie Jina la Shule liitwe GASHAZA shule ya Msingi, na ndo iko hivo mpaka leo. JE Ruhoro hapa hana la kujifunza? Bila RUHORO Ngara tungekuwa mbali sana.
  4. Mheshimiwa RUHORO amekuwa na Roho za Ubinafsi kwa maendeleo ya wananchi kiasi kwamba anaona ni bora kujenga kipande cha Rami cha kuingia nyumbani kwake huku SOKO LA MKIDIDIRI linalolipa Kodi kila siku ya soko likitaka kufungwa kwa kukosa choo. Je nani alaumiwe katika hilo ? Ni halmashauri au Mbunge? Je angeelekeza hela ya Mfuko wa Jimbo kujenga vyoo hivyo angepata hasara? Hakika, tusingekuwa na RUHORO tukawa na Mbunge mwingine yeyote Ngara tungekuwa mbali kimaendeleo!
  5. Amekuwa na ahadi hewa ambazo hazitekelezeki kiasi cha kuwakatisha Tamaa wananchi (waahidiwa). Ni Bora kuacha kuahidi kama hauna uhakika wa kutekeleza, hii ni zaidi ya hekima. Ameahidi kuchangia Tsh 5,000,000/= ujenzi wa Kituo cha Afya Kabanga bado hajatimiza! Ameahidi Tsh 10,000,000/= ujenzi wa Kituo cha Afya MUGANZA bado hajatekeleza! Ameahidi Tsh 2,000,000/= ujenzi wa Kituo cha Afya Rulenge bado hajatekeleza! Ameahidi Ng’ombe Wanne uzinduzi wa Sekondari Mpya ya Murubanga – Nyamagoma bado hajatekeleza! Ameahidi ujenzi wa Vyumba vya Madarasa Shule ya Msingi Nyamiaga bado hajatekeleza! Je anataka kutuaminisha kuwa wabunge wote waliomtangulia walikuwa na ahadi za uongo mithili yake ? Hakika bila RUHORO Ngara tungekuwa mbali sana kimaendeleo.

Jamii ya Ngara inatambua mchango wa Mbunge wetu wa sasa Ndugu NDAISABA GEORGE RUHORO katika:-

  1. Kujitolea kuwasomesha watoto wa Viongozi wa CCM wa kata kama sehemu ya fadhira na mvuto wa kujijengea mazingira ya kura kuelekea chaguzi za mwakani wakati YATIMA, wajane na wenye ulemavu wanazidi kuteseka pasipokuwa na msaada wowote ila ukitokea msiba anajitahidi kutuma wawakilishi.
  2. Kuwadhihaki Wapinzani (CHADEMA) na KUYACHUKUA majibu yao dhidi ya dhihaka zake katika kujiimarisha kiutendaji. Press Conference ya CHADEMA NGARA baada ya tamko lake la kuifuta CHADEMA Ngara ndiyo imegeuka kuwa wasilisho lake ujio wa Katibu Mkuu wa CCM TAIFA Mjini Ngara. Kwa maana nyepesi, mawazo ya wale anaowapinga yamemuimarisha maradufu. Bila uwepo wa Ruhoro Jimboni kwetu hakika Ngara tungekuwa mbali sana kimaendeleo!
  3. KUCHUKUA miradi na vipaumbele vya serikali na kuvifanya kama sehemu ya vipaumbele vyake binafsi kiutendaji. Kwa maana nyepesi anatumia miradi ya umma kupotosha umma kwa kuifanya ya kwake. Mara aseme ameleta sekondari Nyamagoma, mara Bugarama, mara aseme nimeleta Hospitali ya wilaya ya Mbuba vitu ambavyo ni vipaumbele vya serikali.

Mheshimiwa Mbunge wa Ngara Ndugu NDAISABA GEORGE RUHORO anapaswa kutambua kuwa, wananchi wa kupiga kwa mgorigori na kipande cha sabuni wameshaanza kufunguka ubongo. Kupuuza JITIHADA zilizofanywa na watangulizi wake huo ni utovu wa nidhamu.
Ngara Ina raslimali nyingi sana ambazo tungekuwa na Mbunge smart kwa utawala huu wa mama Samia angeziexpose na kuitangaza Ngara kuliko kuitangaza Ngara kwa mambo binafsi yasiyo na tija kama UCHIFU na Passport za kusaka ubunge kwa nguvu.

Faraja ya wanangara itatengenezwa na wanangara wenyewe. Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura linaelekea kumalizika, watu wameshapata nyenzo ya msingi kuelekea uamuzi wa 2024/2025. Hakika Honorable Ruhoro asipobadirisha mtazamo, Jimbo analiachia asubuhi na mapema 2025.

NGARA BILA RUHORO TUNGEKUWA MBALI SANA KIMAENDELEO!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *