Kabanga Mna Diwani Bora, Mfano wa Kuigwa

By admin May 23, 2025
Mheshimiwa Hafidhi Abdula, Diwani wa Kabanga

‎Na, Said Soud-Transit Dar-Bujumbura

‎Asalaaam aleikhum, ndugu pokeeni salamu zangu kutoka Kabanga-Ngara!

‎Mimi ni driver napita tu….ila kwakuwa ni home hapa wacha niseme. Kabanga ya miaka hiyo, si sawa na leo.

‎Hta maandiko yanasema kuhusu Uchaguzi 

‎1. “Chagueni viongozi waadilifu, wacha Mungu, wanaoogopa Allah katika uongozi wao.”

‎Hii inaendana na Qur’an (Surah Al-Baqarah 2:247) ambapo Allah huchagua mwenye elimu na nguvu.

‎2. “Kiongozi mwema ni neema, na kiongozi dhalimu ni adhabu kwa watu.”

‎Hadith: Mtume Muhammad (SAW) alisema: ‘Kiongozi bora ni yule anayewapenda raia wake na wao wakampenda, na kiongozi mbaya ni yule anayewachukia watu wake nao wakamchukia.’ (Sahih Muslim)

‎3. “Muislamu hastahili kumpa madaraka mtu asiye na uwezo au mwaminifu.”

‎Imepokewa katika Sahih Muslim, Mtume alisema: “Atakapokabidhiwa jambo kwa asiye na uwezo, basi subiri saa (ya Qiyama).”

‎4. “Uongozi ni amanah (dhamana); mnapaswa kumchagua yule mwenye uwezo wa kuitimiza.”

‎Qur’an Surah An-Nisa (4:58): “Hakika Allah anawaamuru kurudisha amana kwa wenyewe…”

‎5. “Kura yako ni ushahidi mbele ya Allah – usimchague mtu kwa ukabila, urafiki au rushwa.”

‎Naomba niwapeni ukweli ndugu zangu mliobahatika kukaa na kuishi Ngara…… Sisi huko tulipo tunaishi kwakuambizana ukweli. Na hii ni mbegu nawaachia. Nawapa mifano bila kutaja majina na kata zao,ila mnawajua na mtafanya uchaguzi mzuri.

‎Mifano ya utendaji mbovu wa diwani,na Nawapeni muone kama mtawachagua kuwachagua tena!!!!!!!:,

‎Kutojitokeza kwenye vikao vya baraza la halmashauri

‎Kutopeleka au kufuatilia kero za wananchi wa kata yake

‎Kujihusisha na vitendo vya rushwa au ubadhirifu wa mali ya umma

‎Kutowasilisha taarifa za maendeleo au miradi ya kata kwa wananchi

‎Kutokuwa na uwazi na ushirikishwaji kwa wananchi

‎Madhara ya utendaji mbovu:

‎Miradi ya maendeleo inaweza kusimama au kutotekelezwa kwa ufanisi

‎Wananchi hupoteza imani kwa serikali

‎Ushirikiano kati ya wananchi na halmashauri hupungua

‎Haki za wananchi huweza kupuuzwa

‎Nini kinaweza kufanyika?

‎Wananchi wanaweza kumwita kwenye mikutano ya hadhara kumwajibisha

‎Baraza la halmashauri linaweza kumpa onyo au pendekezo la kumwondoa

‎Wakati mwingine, kura ya maoni inaweza kupigwa dhidi ya diwani

‎Viongozi wa chama chake pia wanaweza kumwajibisha. Siwaagi leo,nitarudi

By admin

Leave a Reply