Vijana, kwa maendelo bra ya Ngara na nchi yako, unahitajika kwenye uongozi. Hivi unayemuita mheshimiwa mbunge leo miaka 7 alikua na hilo koti la ungozi? Alitoka familia inayojulikana na utajiri aliokuwa nao leo alizaliwa naye? Ama aliutoka kwa mama yake? Kama majibu ya haya maswali ni hapana, ni muda wako kuwa kiziwi wa hizo sauti ndani yako zinazokwambia muda bado, hapana haiwezekani, sina hela wala elimu. Hiyo ni sauti ya shetani, ipuuzie, huna la kupoteza zaidi ya kupoteza umasikini, tosa jina lako katika kinyang'anyiro cha uongozi. Pengine anayekupakia simulizi ya kwamba mambo yanaenda hivi na vile anakuzidi umri ama hata kama unamzidi, je amezaliwa na huo uwezo wa kukuhadisia? Hapana, aliweka uoga pembeni akaweka mguu mbele na kutokua na aibu na kugombana hata na wale aliowaita marafiki na ndugu ili awe hapo alipo leo. Uongozi haupewi bali unausaka kwa kila mbinu. Kijana, uoga ndio unaozuwia mafanikio yako. Leo ndio muda sahihi wa kutia jina lako na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa lako. Acha kusikiliza simulizi, tenda kwa kuitia nia ili unufaike na ufalme unaoletwa na nyadhifa mbali mbali. Uongozi unanyakuliwa na sio kuombwa, usitegemee kuna mtu atakuona huku na yeye ana familia na ndugu wanaomtegemea kwani atawaona wao kabla hajakufikia. Acha ujinga kwa kuonwa na jicho la tatu ama la huruma, umeshamuona binadamu ana zaidi ya macho mawili kweli? Acha kuishi na ndoto za mchana, kwa nini uangaliwe kwa jicho la huruma huku na wewe unaweza kujiona kama upo tayari kujifunza na kukosolewa?
Kijana weka kifua mbele na tumia ujana wako kujenga taifa lako kwa manufaa ya jamii yako. Kijana usitishwe, hii sio nchi ya wazoefu tuu ama ya wazee tuu. Hata jasho lako lina nafasi katika ujenzi wa nchi hii, ni muda wako wa kuvuna matunda mema ya kiuchumi kwa kunyakua nafasiza mbali mbali. Acha kutumiwa kama mjaza umati katika mikutano ya wenzio ambao walitia uoga pembeni na kuwania fursa, na wewe pia unafaa na kupendeza zaidi kukusanya na si kukusanywa na kupokea ngojea za wengine. Ngara, Taifa, na Jamii inahitaji mchango wako katika uongozi wako. Ingia leo hata kama unaambiwa hauna jina maruufu, ni jitihada na kushinda uoga vinavyojenga uchumi. Kutumika kama nzi kwenye mikutano ya wengine na kurudi kwenye nyumba ambayo haina bima ya afya, umeme, maji safi ama mazingira magumu ya kimaisha - yote haya yataisha kama ukiingia kwenye uongozi. Acha kuimba imba matatizo kana kwamba viongozi unaodhani unawaperekea lawama wana nia ya kuzimaliza. Wao wamezigeuza fursa ili wananchi waendelee kuona umuhimu wao, wewe kama kijana mwenye uelewa ulimwengu wa leo utatenda haki kwa kuingia na kunyakua nafasi ya uongozi - leo hii kwani kesho haijawahi kufika. Usiwe mwelevu darasani tuu bali na maishani - shiriki kujenga uchimi wa nchi hii kwa kusaka uongozi. Kazi na uamuzi kwako kijana. Tunakuhitaji ung'ae kwenye picha kama kiongozi na sio kama mpiga makofi/mjaza umati kwa walioagana na uoga.
Vijana Msikatishwe Tamaa
Mbinu chafu za kuwatumia ndugu,jamaa na marafiki zimeanza. Kundi la Wanasiasa fulani kwa maslahi yao wameanza kutumia mbinu chafu ziliwemo kuwaita marafiki wa wahombea hasa kundi la vijana kwaajili ya kuwalaghai. Muda huu tayari zoezi linaendelea. Vijana kuweni makini
Muda wa vijana kuongoza ndio huu, mnapendeza zaidi kama viongozi na sio kwa kupokea simulizi kwenye benchi. Hata huyo mnayemuita kiongozi, juzi alikua ni mshaka tonge. Ingieni kwa wingi mnakue nafasi mbali mbali serikarini. Hii ni nchi ya kila mtu, sio ya wazee tuu. Hata mchango wa vijana ndio unaosukuma uchumi wa nchi hii. Ngazi mbali mbali zipo wazi, acheni uoga.
Niwashauri, Vijana hawapaswi kukatishwa tamaa kuelekea uchaguzi, hata kama kuna mbinu mbovu zinazotumika. Hii inaweza kuwa sehemu ya mikakati ya kuwanyima sauti na ushawishi wao katika maamuzi ya taifa. Badala yake:
Waelimishwe kuhusu haki zao za kidemokrasia – wajue kura yao ina thamani.
Wahamasishwe kushiriki kwa amani, kwa wingi, na kwa umoja.
Wapate nafasi ya kujieleza kwa njia halali – mitandao ya kijamii, midahalo, na majukwaa ya vijana.
Wakumbushwe kuwa mabadiliko ya kweli huletwa na ushiriki wao – siyo kwa kuachia nafasi.
Vijana acheni kuishia kuwa wapiga makofi na wakodoa macho kwa viongozi. Ingieni ulingoni, gombea nafasi. Mchango wenu kwa Serikalini unahitajika na wananchi hawatonufika nao mkiishia kukaa benchi na si kuingia kwenye mchakato wa kusaka nyadhifa mbali mbali za uongozi. Nii ni Ngara yenu na ni nchi yenu. Hata kama mtakatisha tamaa kuwa hamna uzoefu, hata hao wanajitapa tapa kuwa nao hawakuzaliwa nao. Ingieni, tuu, mtakosea kosea mwanzoni ila mtajifunza na kuwa wataalamu. Kukodoa macho na kung’ununikia nje ya ulingo wa ushindani ndiko kunafanya vijana waonekane ni mafukara. Acheni kupiga makofi, saka uongozi upigiwe makofi. Hii ndio karne ya uongozi kwani kesho hajawahi kufika ila leo ni leo na leo ndio muda sahihi wa wewe kijana kuwa kiongozi.
Si vibaya kusindikiza, ila mpaka lini? Tengeneza mazingira ili uweze kumudu matonzo ya watoto wako, uwe na mazingira mazuri yenye maji na umeme wa kuaminika, bima ya uhakika ya afya je unayo? Kijana, amka, hii ni nchi yako pia.
Vijana, kuongoza inawezekana, hamkuumbiwa kuwa waongeza umati. Kukosea ndiko kujifunza na hata sio wote wanaongombea wanapesa. Kinachohitajika ni ushawishi na kuwa na watu na sio pesa. Hamna hata siku moja utakua na pesa ya kutosha, wewe tosa jina lako tuu ulingoni, kama sio kushinda, angalau jina litakumbukwa kwenye ujazaji wa nafasi zingine serikalini. Ni dhambi kwa kijana kuendelea kulalamikia kwenye benchi. Ingia kwenye utawala kwa manufaa ya jamii yako. Huu ndio muda sahihi kwa kijana kuongoza.
Vijana mpo wapi kwenye uongozi ama uoga umewafanya muwe wasindikizaji. Kwenye picha mnapendeza ila inapendeza zaidi mkiwa kwenye uongozi. Mnaruhusije jimbo liongozwe na watu wasioona umuhimu wa teknolojia na hata smart phone (simu janja) hawana? Kama jamii inaweka order kwa mzigo uliopo Dar Es Salaam na ukaletwa na vijana mpaka Ngara, inakuaje uongope kujaribu kitu kipya kama uongozi kwa jamii yako? Sio pesa, weka uoga pembeni, tosa jina lako na lolote litakalotokea litakua tokeo. Acha kuwa mpiga makofi na mpokea ngojera toka kwa wengine. Ni vizuri na wewe uweze kunufaisha jamii kwa matumizi ya teknolojia kama kiongozi. Kijana anauwezo wa kufikiria haraka, kufanya uamuzi haraka, kutatua changamoto haraka ili mzee anayekuongoza leo awe na maisha bora kesho. Sasa acha uoga, ingia kwenye nyang’anyiro kijana. Kama ujenzi wa soko, kituo cha mabasi umekwama, ingia uzibue kinachosimamisha maendeleo ambayo Ngara inahitaji. Leo na sio kesho ndio muda sahihi kwa kijana kuongoza. Jana uliambiwa kijana ni taifa la kesho, je umeshaiona kesho? Ila leo kwenye mikusanyiko ya siasa upo, sasa usikusanyike kukodoa macho ama kuvuruga mikutano ya wengine, ongoza. Leo ndio muda wako, anayekwambia kijana ni wa kesho, mtarifu kuwa na yeye kesho atafaa kuongoza, akupishe ulete maendeleo kwa jamii. Kuishi na huu masikini tulionao maishani ni kutokana na uoga tuu, ongoza leo ili utokomoze uhaba unaokwamisha wana Ngara. Kijana, muda wa kuongoza ni leo, usikatishwe tamaa.