MENEJA WA TRA AHUKUMIWA KUFUNGWA GEREZANI MIAKA 20

By Na Mwandishi Jun 30, 2026

Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Kigoma imemhukumu kifungo cha miaka 20 gerezani aliyekuwa Meneja wa TRA Wilaya ya Kibondo, Bwana Irving Bagasheki baada ya kukutwa na hatia katika makosa mawili ikiwemo kupatikana na nyara za Serikali isivyo halali ambazo ni meno ya tembo mawili yenye thamani ya shilingi milioni 52.

Hukumu hiyo imetolewa Juni 29, 2026 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma Aristida Tarimo mbele ya jopo la mawakili wa Serikali wakiongozwa na Telix Kwetukia baada ya Mahakama kujiridhisha kuwa ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka ulithibitisha kosa hilo bila kuacha shaka lolote.

Mnamo Julai 01, 2024 Bwana Arving Bagasheki mwenye umri wa miaka 40 alikamatwa katika ‘beria’ ya Kihomoka wilayani Kakonko mkoani Kigoma akiwa kwenye gari ya Serikali yenye usajili namba STL– 7274 akijaribu kusafirisha meno hayo ya tembo mawili yenye thamani ya shilingi milioni 52 kinyume na sheria za nchi.