Ngara: “Mkilazimishwa kula kuleni ila msiwape Kura” Askofu Severine Niwemugizi

By Titho Philemon Jul 29, 2024

Akiongea na Waumini pamoja na wanajamii katika Kanisa la Mt. Mathias Mtume Parokia ya Murusagamba katika Misa Takatifu ya Upadrisho Jumapili ya Tarehe Agosti 28, 2024 Askofu Niwemugizi ameiasa jamii kuichukia Rushwa ili waweze kupata viongozi wenye ueledi na wenye uwezo wa kuisaidia jamii.

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge Ngara Mhashamu Askofu Severine Niwemugizi ameiasa jamii ya Ngara pamoja na Watanzania wote kuacha tabia ya kushawishi kupewa Rushwa hususani katika hiki ambapo taifa linaelekea uchaguzi wa serikali za mitaa October 2024 na Uchaguzi Mkuu hapo mwakani.

Aidha, Niwemugizi amewasihi wanajamii kupokea chochote kutoka kwa wanasiasa wapendwa Rushwa pale tu watakapoona kuwa kukataa kupokea hongo kunaweza kuwapelekea madhara makubwa dhidi ya watoa rushwa na kwamba baada ya kupewa kula wale ila wasitoe kura.

Akiangazia zoezi zima la kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura linalotarajia kuanza August 5 mwaka huu Askofu Niwemugizi amewataka waumini wote kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo ikiwa ni sehemu ya utiifu, kutimiza wajibu na kuheshimu mamlaka.

Kwa upande mwingine, Askofu Niwemugizi amekemea tabia ya baadhi ya wanasiasa kumdhihaki Mungu pale wanapothubutu kumhusisha katika vitendo vyao viovu. Katika kulisemea suala hilo Askofu Niwemugizi ameeleza video iliyokuwa ikisambaa mtandaoni ikimhusisha mmoja wa wanasiasa wakongwe hapa nchini akijinasibu kuomba msamaha baada ya kuiba kura, kitendo hicho ni kibaya sana na ni kumdhihaki Mungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *