Katika pita pita za humu Ngara, tunaona upendo, undungu, na maendeleo. Upendo na Undugu ni vitu vinavyoelezeka na kufahamika kwa wengi. Ila inapokuja kwa neno maendeleo, wale wenye ubunifu na uelewa mzuri wa lugha, basi wanaweza kuelewa. Neno maendeleo si msamiati kihivyo ila hata ghali ikiwa imepungua ama ongezeka, tunasema yote ni maendeleo ama ni matokeo. Tuchukulie mgonjwa, maendeleo yanaweza kuwa yamekua mabaya ama yamekuwa mazuri kwani dawa tunategemea ilete maendeleo mazuri ila muda mwingine mambo yanakua sivyo.
Ila wanaposema Picha ni nusu ya Kuonana maana yake ni nini? Ndio kujuana, kujenga undungu ama basi tu ni kutulia pamoja kwa sekunde kadhaa wakati kamera inavyafuliwa. Ndugu msomaji, kwa picha hiyo hapo juu inakuletea hisia gani? Kuna undugu hapo? Kuna Upendo, ama kuna kujuana? Kujuana kwa mazuri ama mabaya?
Kuna maisha baada ya siasa. Jumatatu Njema!