Restitutha Binambi Ajitosa Kwenye Nyang’anyiro la Ubunge – Ngara

By admin Jun 11, 2025
Wana Ngara, naomba mnisikilizeni, nimeamua kutangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Ngara baada ya kuona utoto ni mwingi wa mbunge aliyepo. Ametoa ahadi nyingi na hata moja haijakamilika. Tusioneanea aibu, hapa Ngara umasikini wetu unatokana na kuendekeza uoga. Hatuambiani ukweli, asema Restitutha Binambi akiwa anahutubia wandishi wa habari. Kusema ukweli hata kama unauma ni moja ya nguzo muhimu katika uongozi. Ndaisaba Ruhoro, mbunge anayemaliza kuwakilisha Jimbo la Ngara Dodoma hafai tena kuwa kiongozi. Kuna wana Ngara wengi wanaofaa zaidi, mie nikiwemo. Hivi wewe ama tungesimamisha mtoto wa darasa la nne hapa Wilayani na kuuliza tano bora aliyeyafanya Ruhoro hapa Wilayani Ngara zaidi ya kujijengea gorofa, unaweza kuyataja? Na kuelezea jinsi yanavyoinufaisha Ngara? Kama utasita sita kuyafikiria, ni dhahili kuwa miaka mitano Ruhoro aliyokuwepo Bungeni haijaletakitu chochote Ngara zaidia ya uwepo wake kama formality. Ndio mama mimi Restitutha Binambi nimeamua kuingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Ngara ili Ngara ya Kesho iwe njema kuliko hii iliyopo. Pamoja tunaweza na nategemea ushirikiano wenu kwenye safari yangu ya kuinyakua na kuiwakilisha Ngara Bungeni Dodoma.

MFAHAMU ‎RESTUTA BINAMBI – MGOMBEA UBUNGE  JIMBO LA NGARA

Restitutha Binambi Ataka Kumng’oa Ruhoro

Aweka Kifua Mbele kuongoza wanawake wenzake

Ngara chini ya uongozi wa bi Binambi, kero ya maji itakua historia kwani Atachimba visima wilaya nzima

Amebobea kwenye uongozi, tokea alivyokua chuoni Dodoma

Restitutha Binambi, mbunge wa Ngara mtalajiwa akiongea na wandishi wa habari aliuza, mnakumbuka mgombea ubunge Ndaisaba Ruhoro alivyotoa ahadi nyingi na hamna hata moja aliyoitimiza? Nimesikitishwa kuona kuwa maneno ya Ruhoro akiwa mgombea yalikuwa matamu kwenye masikio ya wana Ngara ila leo hata hakuna kimoja kinachoweza kusimamia uongozi wake kama asiposhinda awamu nyingine. Nimeamua kugombea ili niokoe Ngara na niboreshe maisha ya wana Ngara. Hata ahadi ya kupanda Kawaha Ngara Ruhoro ameshindwa kuitimiza kikamilifu. Chini ya uongozi wangu kama mbunge, Bi Binambi amewambia wandishi wa habari, nitahakikisha upandaji wa kahawa umekamilika, nitaleta mbolea na kuhakisha kuna maji ya kutosha. Kipindi Ruhoro anagombea aliahidi kuwawekea vijana fursa mbali mbali, je ni vijana wangapi wanafanya kazi hata kwenye kiwanda chake za alzet? Je ile studio ya wana music ipo wapi hapa Ngara ama imenufaishaje wana Ngara? Kwa mabinti kama sie ametugeuza mama wa watoto wake ila tunataka ajira na sio ahadi hewa. Jimbo la Ngara chini yangu, tutatia kipao mbele katika ajira, na kuweka usawa kwenye jamii zetu. Hakika nitafanya kazi bega kwa bega na Mheshimiwa Oliver Semuguruka kuhakikisha wanawake tunakua mstari wa mbele katika ujenzi wa Taifa.

‎Kwa sera zake thabiti na maono ya kweli ya maendeleo, Restuta Binambi anaonyesha kuwa ni chaguo sahihi kwa uwakilishi wa wananchi wa jimbo la Ngara.

Restitutha Binambi: Wana Ngara kuongoza sijaanza leo na nimeongoza wanaume na wanawake. Ni muda wa kumpuzisha Ndaissaba Ruhoro ili nisafishe Wilaya Yetu. Weka imani kwangu na tutafanya mazuri tuu tukiwa pamoja. Nipo tayari kuwa mtumishi wenu. Changua Restitutha Binambi kama mbunge wako. Mimi ni tofauti, sitotoa ahadi ambazo sitotimiza.

‎ Juni 11, 2025, aliwasilisha maelezo ya kina kuhusu malengo na dira yake ya kisiasa. Wananchi wamemuelewa na wengi wameonesha imani juu ya uwezo wake wa kuleta mabadiliko chanya.

💡 Restitutha ana dhamira ya kweli ya kuipeleka mbele wilaya ya Ngara kupitia uongozi jumuishi, uwazi na usawa wa kijinsia. Uwakilishi wake hautakuwa tu kwa niaba ya wanawake, bali pia ataleta nguvu mpya kwa kundi la wasichana na kuwahamasisha kujiunga na siasa – kama anavyofanya Oliver Daniel Semuguruka, ambaye pia ni mfano bora wa uongozi vijana.

Restitutha Binambi, Mgombea Ubunge Jimbo la Ngara, aahidi kuwapa kipaombele wanawake na kushughulikia kero zinazokwamisha Wilaya ya Ngara kimaendeleo. “Ndio, kuna kero nyingi hususani sie wanawake,” ila msiwe na wasi wasi, tutawaongoza hata wale wanaojidai hawawezi kuongozwa na wanawake. Wanawake tunaweza, tusizubae kwenye huu mchaka mchaka, uongozi ni wetu na uongozi unapokua mbaya, sisi ndio tunabaki na watoto na kero zote za nyumbani. Tufunge mikanda katika kusaka vyeo mbali mbali. Maendeleo hayatopatikana kama tutazubaa na kuwaachia wengine uwanja kwenye uchaguzi huu.

🤝 Wananchi wa Ngara wanapaswa kumuunga mkono binti huyu mwenye maono, bidii na moyo wa uzalendo. Ni wakati wa kuamini katika nguvu ya vijana na wanawake kujenga taifa letu.

Restitutha Binambi, kiongozi thabiti, fahari ya Ngara. Tembeo la uhakika, chaguzi sahihi kwa Ngara
Restitutha Binambi, Wanawake Tunaweza!!! Niunge Mkono tusogee mbele. Ngara Njema Iko Mbele Yetu, Pamoja tunaweza.
Restitutha Binambi, Mgombea Ubunge Jimbo la Ngara ameahidi kutokua kama wale wanaotoa ahadi nyingi na kushindwa kutimiza hata moja kikamilifu. Halidhishwi na utendaji kazi wa mbunge aliyepo na sasa kama binti shujaa afanya uamuzi wa kuinanua Ngara yake kutoka kwenye umasikini.

Resitututha Binambi, Mwenyekieity wa Kamati ya Binti UVCCM Seneti Mkoa Dodoma
Hakuna wasi wasi inapokuja katika swala la uongozi kwa Restitutha Binambi. Kama mmoja wa binti UVCCM Seneti, utendaji wake umetukuka.
Restitutha Binambi, binti supavu, msomi, kiongozi kamili ambaye anakosa usingizi kama jambo lake hajalikamilisha. Yupo tayari kuwakilisha Jimbo La Ngara kama Mbunge. Anategemea kura yako, mwana Ngara. Wanawake wanaweza.

By admin

Leave a Reply