Tamaa za Kuutaka Urais Zimeanzia Kwenye Uchifu

By admin May 7, 2024
Rais Samia Suluhu Hassan, na kwa jina la kimira: Chifu Hangaya

MTAKA YOTE KWA PUPA HUKOSA YOTE, MBUNGE ATAKA KUPEWA UCHIFU KAMA RAIS

Hali ilipofikia Ngara, Dharau za Kijana tuliyempa dhamana zinatosha kumpumzisha. Mitandaoni kila kukicha ni kebehi,kejeli na dharau za kila rangi!!!

Tuna Mbunge wa ajabu haijawahi kutokea.

1. Aliwahi kuratibu zoezi la kusambaza picha kwa wafanyabiashara,watu maarufu na Ofisi kadha wa kadha ili zipambwe kutani kama ilivyo Picha ya Rais.

2. Mara kadhaa ameratibu shughuli za kuwakuta Isha watu hasa Viongozi wa kada mbalimbali kutafuta uubgwaji mkono.

3. Hali imefikia pabaya,ameratibu zoezi la kuzikutanisha familia za Machifu wa Bugufi na Bushubi. Lengo ni kutaka atawazwe kuwa Chifu, na Mlezi wa familia za Machifu Balamba na Nsolo.

Lengo, ni kila aina ya Sifa aliyonayo Mheshimiwa Rais wetu awe nayo. Na hii ni tahadhari!!!!!!!!

Kwa hali ilivyo, ipo siku tutaamka, tutakutana na Kauli ya Kutawazwa kama siyo kuapishwa kuwa Rais…hii ni dharau. 

Kama kila kilichofanyika Ngara, hawezi kutambua mchango wa Serikali, Mamlaka na nguvu ya Chama badala yake anajitanguliza atashindwa nini????

Kama Ubunge tuliompa haumtoshi, na anataka Uchifu itoshe kusema basi. Tumpunguzie majukumu, akalee watoto kwa mjomba na shemeji zake

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *