Safari ni safari. Hata iwe ni kwa miguu, kwa kutambaa, ama kupaa…. cha muhimu ni tuwe tunapiga hatua.
Tulipoanzia ni mbali, na hapa tulipo tumepafika kwa kuwa tumejongea na kujikuta hapa. Tulipoanza tulikua wengi na tulishibishwa ahadi eti tutajengewa hiki na kile. Tulikua na kifua cha Mheshimiwa mwenyewe. Ahadi zilikua nyingi na tulipojaribu kuelekeza na kuweka mambo sawa, wengine tulijikuta tunachezea kichapo rumande kilichotuacha na makovu ambayo sasa ni ishara ya kutoridhishwa na hatua zilizokua zinaahidiwa midomoni zikishindikizwa na jitihada nyingi ila na bigenda.
Mara tukapatiwa mchuma ambao ulikua unakufa kufa mara kwa mara. Nia za kwenda vijijini kutafuta habari zikafia kwenye picha kwani kuna kipindi tulikua tukikata kona tuu, mchuma unazima. Tulipotaka kuutumia, kina waliokua karibu na Mheshimiwa na wao walikua wanasikilizwa sana na wanatumia kiburi chao mpaka kazi hazifanyiki tena. Ila basi tena, kwa kuwa ukaribu na urafiki kwa Mheshimiwa ulikua una uzito kwenye munzani, wengine waliokua na maoni walikua hawana kibesi na hatusikilizwi.
Ila kuna wengine waliambulia kuvaa sare ambazo hatujui zimeishia wapi. Katika picha tulionekana vizuri ila katika taaluma ilikua ni vichekesho. Tulihudhuria vikao mbali mbali, hadi pale rais alipobahatika kuzuru Wilani Ngara tulihudhulia ila sasa kamera zetu zilikua hazioni ndani na hatukubahatika kurusha habari yeyote. Sifa nyingi tulipewa, meno yalingaalisha, na mapicha kibao kibao. Kuona Upepo ulikua kwetu, basi tukajua journalism ni kusikiliza waheshimiwa tuu na kuandika kile walichotaka kisikike.
Tuliahidiwa mishahara minono na tulipoona ni ahadi hewa, tulianza kupenyuka penyuka kama punje za mahindi kutoka kwenye gundi. Ila Gunda alipendeza, na alishiriki katika program mbali mbali tuu. Wengi wetu tulikua tumesahau kama taaluma zetu ilikua ni ualimu na tukajikuta tunarudi darasani. Mara tukaambiwa eti shule hazina vyoo. Yaani ilikua kama vile ni kipindi cha ukoloni ambapo vitabu vianza kuandikwa eti huyu na yule kavumbua kitu fulani. Tulijua kuwa vyoo, madawati, maji na vinginevyo ni matatizo yaliyokuwa yameikumba Wilaya Yetu. Ila sasa ukiyaongelea ungeonenakana msaliti.
Utaongelea hizi changamoto huku hata tunapoita nyumbani hatuna umeme wala maji ya kuoga? Wengine tulikua tunaonga mara moja moja kwa wiki kupelekea ugonjwa wa UTI kuwa ni sawa tuu. Kipindu pindu, kolera na mangojwa mengine yameshazoeleka na nisehemu ya maisha yetu hapa. Sasa tupige makelele eti tunataka mabomba nyumani kwetu tuachane na haya magonjwa ambayo yalikua yanatupatia kajirikizo ka kutokwenda shule jamani? Nani anataka awe anakwenda shule bila likizo?
Kwa kweli muda tumetoka mbali na bado tunaendelea na safari. Leo tunaambiwa eti piki piki na lile gari letu vimepotea. Baadhi ya nyenzo za kazi pia zimegawanywa gawanywa na kusambalatika. Hata ubao wetu wa Ngaratv.com haubandiki tena habari moto moto kama awali. Ila wawili-watatu tuliombaki tunaendelea kuhakikisha kibari hakizimi kabisa. Wale waliokuwa wanajitamba kwa ukaribu wa Mheshimiwa wanatusingizia kuteka dot Com na kuitawala tuitakavyo. Kama wao walikua wanapewa mazawadi mbali mbali kama magari, viroba, mitungi ya gesi, na hata wake wa kuoa, sie tubaki na nini? Si tumewaachia Ngara yenu tukakimbilia sehemu zingine ambapo tupo salama kwani hata tungebaki Ngara Mheshimiwa hakutujari maana damu yetu ilikua haivani. Wengine tulikumbushwa kuwa asili yetu si ya hapo Ngara, eti ni taaluma ya ualimu tuu ilitufikisha huku ama eti hatuna uchungu na hapa kwani hatukuoa kutoka kwenye familia zenye jina. Wengine tulitukanwa na kukejeriwa kuwa hata sifa ya kuitwa Muhutu, Mtusi, na kabila zingine za hapa hatuna. Sasa tukaona tujibakie kimya kwani huu ukabila nao naona kama unatenga jimbo zima baadala ya kutufuma na kutuunganisha tukajenga Ngara yetu pamoja.
Ndio maana tukaona tuendelee kuleta habari hapa Ngaratv.com na tuendelee kubebesha kibatari mpaka pale Jimbo la Ngara litakapookolewa tena. Tuendelee kusambaza habari hasa kwenye vyombo vya kuaminika kwani huku tulipo tunaishiwa kukisiana na kuitana majina eti wewe na yule ni mvujishaji/msambaji wa habari. Ila hakika ukweli unavujishwa na mambo yanasomwa na walengwa. Ngara yetu tutaendelea kuilinda hata kama tunaendelea kujisogeza kwa Mheshimiwa na kumtumikia. Mwisho wa siku lazima tule ila sasa haki itendeke na habari ziwafikie walengwa. Leo tuliobaki Ngaratv.com tupo ngangari na hakuna kilichoibiwa kama ilivyotajwa hapo awali.