Faini ya Milioni 4 – Katibu wa Mbunge wa Ngara

By admin Mar 2, 2024

Na Auntie ARV, Ngara Mjini

Kwenye mitandao kadhaa ya kijamii, kumekua na minong’ono juu ya kesi zisizokua na kichwa wala miguu, kutengenezwa na kubambikiziwa watu mbali mbali Wilayani Ngara. Inasemekana wanaobambimiziwa kesi ni wale wanaojikuta wako ukurasa tofauti wa kimtazamo na Mheshimiwa Mwenyewe.

Aliyewahi kuwa katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ngara mheshimiwa Juve Jeventus ameshia akiitwa mahakamani kwa kile kilichodaiwa kumuaibisha mwenyekiti wa kijiji cha Ibuga. Kulingana na mashitaki yaliyopo kwenye nakala za mahakamani,  Mwenyeketi wa Ibuga, Bwana Morris Ndala, anadai amedharauliwa (defamation) kwa kuulizwa aelezee “mafanikio yaliyopatikana tangu alipochaguliwa kuwa mwenyekiti” na ndugu Juventus Juvenary. 

Kama mwandishi wa habari, ndugu Juventus Juvenary wa Juveilla TV aliambatana na wandishi wengine wa habari kutoka Simamia TV kwenda Ibuga ambapo Mwenyekiti wa kijiji hicho alionekana akikimbia waandishi wa habari. Aliishia kumstaki ndugu Juvenary Juventus peke yake, jambo ambalo wana Ngara hususani wana Ibuga wamejiuliza kama Uhangaza wake ndio umemlemea Ndugu Juventus na kuburuzwa mahakamani. Kama wandishi walifanya kosa kwa kujaribu kutangaza mazuri ya Ibuga, basi wandishi wote watatu walioshiriki kumuuliza maswali Mwenyekiti wa Ibuga ingekua vyema wote wakafikishwa mahakamani. Kazi iliyofanywa na wandishi hawa imewekwa mwishoni mwa hii makala kwa manufaa ya msomaji. 

Hali ya kuchekesha na kusikitisha ndio iliyoonekana mahakamani. Ni hali ya kuchekesha kwa kuwa mleta mashitaka alionekana amechoka na kulalamika kwani hakujua hata sura wala jina la aliyekuwa anamshitaki. Hakujua hata undani wa kesi iliyokuwepo mbele yake na wala hata sahihi yake haikuonekana mahali popote kama mleta mashitaka. 

Hii kesi ilikua inasikitisha kwani ilimuabisha mleta mashitaka na kumgeuza mfurahishaji (entertainer) kwani mtaani na kijijini kwake anavishwa kofia ya uheshimiwa, uenyekiti ila mahakamani yeye ameorodheshwa kama mleta mashitaka, mashitaka ambayo hata alikua anashindwa kuyaelelezea. Alipoulizwa ni wapi ama ni neno gani kwenye ile program ilikuvunjia heshima na ni hasara gani imetokana na huo uvunjifu wa heshima yako, Mwenyekiti wa Ibuga alionekana kama anashangaa na kutojua kinachoendelea na kuishia kudai kuwa yeye anafata maelekezo kutoka juu.

Hakika Mwenyekiti wa Kijiji cha Ibuga mara kadhaa alionekana kutojua kesi iliyikuwa ikiendelea. Hata alikua haelewi kwa nini jina lake limeorodheshwa kwenye nakala za mashitaka kwani alipoulizwa, alidai ni mwanasheria wake ametayalisha nakala zote na yeye aliwezeshwa tuu kufika mahakani na hataki kumuudhi mtu, kwa hiyo amefika mahakamani kutii amri tuu.  

Akiongea na Ngara TV, mtuhumiwa bado anashangaa na bado haelewi kiini cha hii kesi. Nimeamua kufika mahakani kwa heshima ya mahakama, bwana Jeventus Juvenary alielezea, ila sielewi hawa waliopo nyuma ya hizi kesi wananufaikaje kama hata program nzima inaonyesha kilichotokea na mleta mashitaka hawezi hata kuchambua neno lolote lililoshusha hadi ya uenyekiti wake. Inafurahisha kuona uenyekiti unatajirisha mtu kuliko hata udiwani ama ubunge. 

Tulipojaribu kufanya utafiti wa hii habari, watu wengi hawakutoa ushirikiano kwa dhati kwani walidai hawataki wajikute ukurasa tofauti na waliyemuita Mheshimiwa Mwenyewe. Ila wamesema bwana Juventus amesisitizwa afanye maongezi na mwanzilisha kesi ili “wenyewe wakubaliane na wayamalize nje ya mahakama”. Inasemekana aliyekuwa akidhamini gharama za kuendesha kesi alikua analalamikia ukubwa wa gharama za kuendesha kesi na kesi kuendelea kutafuna muda bila kesi kufikia kikomo. 

Waliokaribu na anayetajwa kama Mheshimiwa Mwenyewe alisikika, wana audio recordings, akitoa maelekezo kuwa wamalizane nje ya mahakama kwani mwanasheria alikua analipwa kitu kama laki tano (5) kila anapoonyesha sura yake mahakamani. Mwenyekiti wa kijiji cha Ibuga alikua anapewa pesa za nauli tuu. Mwenyekiti wa kijiji cha Ibuga alikua akipongezwa kwa uzalendo wake tuu na alipokulizwa kama ilikua ni sawa kusikiliza na kutii amri kutoka juu, Mwenyekiti aliamua kutojibu kitu. Pengine uzalendo na utiifu usiopimwa na kutathiminiwa unaleta mlo na heshima kwa wana Ibuga wengi hususani kwa mke na watoto wake. 

Kwa mtazamo wa waliokuwa wakifatilia hii kesi wameelezea kilichokua kikiendelea kama Mwenyekiti wa Ibuga amejikuta akiingia kwenye “choo kibovu ambapo asipoangalia atajikuta ametumbukia shimoni”. Waliendelea kusema hizi safari za mara kwa mara za kuja mahakamani zilimchosha kwani anasafiri mwendo mrefu kutoka Kabanga. 

Wapelelezi walipotumwa kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Ibuga kupata mawili matatu juu ya kesi aliyokuwa ameifungua dhidi ya bwana Juventus Juvenary alishindwa kuelezea kwa nini kesi imefunguliwa kwa mwandishi mmoja tuu huku walikua waandishi watatu kutoka vyombo viwili tofauti tofati. Mwenyekiti wa kijiji cha Ibuga alidai kuwa hii kesi ina marashi ya kisiasa na haelewi kwa nini anaendelea kwenda mahakamani bila kulipwa huku wanaonufaika ni wengine. Hakika waliofanikiwa kugeuza kesi kuwa mradi wanafaidika huku wanaleta mashitaki wanakubwa na kitendawili cha kutoa maisha bora kwa watoto wao na wakazi wa Kijiji Cha Ibuga.

Aliyetuhumiwa na kupewa hukumu ya kulipa milioni nne naye alikua na mengi ya kuchangia. Ndugu Juventus Juvenary alidai kuwa kwenye makaratasi sawa wameshinda, na kudai sasa ndio watakuja kubeba mke na kunipora watoto ama vipi kwani  sina hata laki moja mfukoni. Waendelee kumpatia nauli tuu za kuja mahakamani tuu. Itakua vizuri mdhamini asiishie kumlipa mwanasheria tuu bali alipe muda ambao tumepotezea mahakamani. Yaani tunashindwa kuboresha huduma za kichumi huko kwetu ili tutoe malezi bora kwa familia zetu. Tunashinda kupigana vikumbo mahakamani kana kwamba kipindi cha upigaji kura tutaorodhesha ni mara ngapi tuliburuza wana Ngara mahakamani, alielezea Ndugu Jeventus. 

Hakika mbio za Mahakamani zimegeuza mahakama kuwa kumbi ya entertainment. Zimeonyesha ubora wa uongozi na hasara za kushindwa kufanyia kazi shauri zinazoletwa. Kama anayeshitaki hawezi hata kuonyesha kipengere kilichomuudhi, na malalamishi yanapokelewa na kufikishwa mahakamani na yule anayejiita mwanasheria, basi vyuo vyetu vinapotosha watoto wetu huko mashuleni. Kutia jina la kampuni na mihuri kwenye kile kinachoitwa kesi bila kukipima ni kuonyesha kuwa malipo ni matamu hata kama kinacholipwa ni upotoshaji na aibu kwa mahakama na wateja wote wanaotegemea hiyo ofisi. Kuna maisha baada ya siasa. Usiruhusu Siasa zishushe hadhi ya ufanisi wako kazini na wajibu wako kwenye jamii.

Video:

Video ikionyesha Mwenyekiti wa Ibuga akikimbia wandishi wa Habari wailiotembelea kijiji chake cha Ibuga. Cha ajabu ni mmoja kati ya wandishi watatu aliyefikishwa mahakama na Mwenyekiti huyo wa Ibuga. Mwenyekiti wa Ibuga ilibidi awe anasaidiwa nauli za kuhudhulia kesi mahakamani ila kitendawili ni wapi ametoa hela za kufungua kesi na kuwa anamlipa mwanasheria laki 5 kila siku atakayokuwa anahudhulia ama kuonyesha sura yake mahakamani. Kwa kweli Wilayani Ngara kuna ya kushangaza, kusikitisha na kuburudisha.

Kulingana na certificate ya mahakamank, bwana Juventus Juvenary amelazimishwa alipe milioni 4 kwa Mwenyekiti ambaye alishindwa kuonyesha umuhimu wake kwa kijiji cha Ibuga kama mwenyekiti wa Kijiji. Hakika kama mtu anajipatia milioni nne, 4, kwa kukimbia majukumu yake, nasi huko Kabanga ni bora kuwa Mwenyekiti wa Kijiji kuliko kuwa Diwani wa Kata.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *