Miezi kadhaa iliyopita, Wilaya ya Ngara ilipata umarufu katika vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa baada ya mbunge wa Ngara, Mheshimiwa George Ruhoro, kuagiza wakazi wa Ngara kutundika picha yake majumbani mwao hususani sebureni. Agizo hili liligeuka uwa kichekesho kwa wana Ngara, na wale wanaoishi nje ya himaya ya mbunge aliyetoa agizo hilo. Wakazi wa Ngara walipuuzia hilo agizo na walisikitika kuona wanaletewa picha na si maendeleo kama walivyokua wakitegemea kutoka kwa muwakilishi wao.
Miezi kadhaa baadae, baadhi ya Wanangara walikusanywa nyumbani kwa kiongozi huyo na kuzawadiwa vitu mbali mbali. Ni zawadi ambazo zilitia aibu na pengine zilivunja taratibu za utawala, uongozi, na chama kilichomuwezesha kuwakilisha wananchi. Zoezi la kutoa tuzo mbali mbali lilihofiwa kuwa na doa kwani waliokaribishwa walipokonywa simu zao pale walipokuwa wakiingia ukumbini ili ushahidi wa aina yoyote ukosekani. Waliokaribishwa hawakuruhusiwa kuchukua picha wala video wa kilichokua kikiendelea. Mule ukumbini, kuna waliopewa fedha, mitungi ya gesi na wengine kuambulia pombe, vilevi vya aina mbali mbali. Baadhi ya hizi zawadi ni hongo ambazo zinavunja taratibu za kitasisi na pengine sheria zkadhaa za nchi.
Video: Rais Samia akielezea njia mbali mbali zinatumika kama hongo na wanasiasa.
Maamuzi ya yupi akaribishwe na zawadi ipi ende kwa mtu fulani ni jambo lililomuhusisha Mbunge wa Jimbo la Ngara. Ila uandaaji na uendeshaji wa shughuli nzima wakati wa haya matukio ni wajibu uliotimizwa na wasaidizi wa Mheshimiwa. Baadhi ya hawa wasaidizi wamebarikiwa kuwa na ufahamu na busara wa kujua taratibu na sheria zilizokuwa zinakanyagwa kutokana na unyemela uliokua unatokea. Hawa wasaidizi walijitoa kwa hali na mali ili wamfurahishe boss wao.
Pale mambo yalivyokwenda kombo na pengine uhalisia kutofichika tena, baadhi ya wasaidizi waliamua kujipumzika na kuachana na sikio lisilosikia dawa. Uamuzi wa kujiengua ni swala ambalo halikupokelewa kwa mikono miwili na Mheshimiwa Mwenyewe.
Uamuzi wa kuacha kazi kwa Mbunge hukuwa mwepesi kwa timu nzima. Kwa wale wanaothamini uhai na usalama wao, amuzi la kutoendlea na usaidizi ni swala ambalo limeleta hofu na gharama kubwa kwa wale wanapoamua kuachana na siasa na kujishughulisha na mengineo.
Imekua ni shida pale wasaidizi wa Mheshimiwa wanapoacha kazi ama pale wanapotofautiana naye kimawazo, alisema Mwana Ngara mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe. Wasaidizi wameihama Ngara kutokana na hali ya kisiasa iliyopo wilayani ambayo inasababisha maisha yao kuwa magumu wanapoacha kumtumikia mbunge wa Ngara.
Wale ambao hawakuona umuhimu wa kukimbia kwao wamejikuta wakitegua mitego mbali mbali na muda mwingine wakifikishwa mahakamani. Baadhi ya wasaidizi wa Mheshimiwa walidai kupewa ahadi ya kupewa Milioni tano – tano kama waachana na ndoa zao na kuowa wahangaza. Hawa wasaidizi walikua wameowa wanawake ambao asili zao si za Ngara. Walipopuuzia hizi ahadi, basi mishahara yao ilikua haitoki kwa wakati uliotarajiwa na walipoulizia moja ya kikwazo walichopewa ni kutoowa Mwana Ngara.
“Aisee ndani Ngara ambapo ndipo uasili wangu ulipo, sijawahi kufikiria mwanaume mwenzangu atakua na uthubutu wa kunichagulia pa kuowa ama kutumia ukabila katika kuamua lini na kiasi cha mshahara nitakacholipwa. Sikudhani kwenye ardhi ya mababu zangu, ardhi yangu ya asili ningejikuta natetea haki ya mke niliyemchagua mwenyewe ama hata kutetea familia yangu na yote haya kutokana na na kujitoa kwa hali na mali ili kijana mwenzangu aweze kuwakilisha jimbo letu Bungeni. Huyu ni mtu ambaye ukipishana naye kimawazo unageuka kuwa adui yake.
Vijana waliofurahia kuongozwa na kijana mwenzao leo wanajuta hata kujihusisha na siasa. Vijana walijinyima na kujinyima usingizi ili kiongozi wao ang’are kwa kutengeneza mazingira mzauri nyumbani ili Wilaya ya Ngara isonge mbele kimaendeleo. Vijana wanaoonekana walivamiwa, kuingizwa mahabusu na walitoka sero na makovu mwilini; wale wasaidizi walioonekana maarufu wamechongewa kesi na kufikishwa mahakamani. Vijana wengine walijitolea hadi dakika ya mwisho ya maisha yao.
Itakua ni ukatili kutotambua mchango wa wasaidizi wa Ruhoro, wasaidizi wote walikua hai ama kutangulia mbele ya haki. Iwe walisaidia kama madereva, wbeba makali migodini, ama waanzilishi wa taasisi mbali mbali ambazo zilizamilia kumrushia Mbunge pambio na kumsogeza karibu na wananchi. Leo vijana waliobaki ndio wanaporwa nyenzo za kazi na kufukuzwa kama mbwa. Wanakumbushwa mamilioni waliyolipwa kama stahiki za jasho lao kama mishahara kuwa ilikua ni misaada tuu waliyokuwa wanapokea. Misaada huhitaji kuhangaikia na kuacha familia nyumbani ili mradi tuu boss ang’are. Hizi ni stahiki ambazo zinategemewa na mfanyakazi na zinatakiwa kulipwa bila kujari jinsia, kabila, ama undugu uliopo kati ya muajiri na muajiliwa.
Kushindikana kwa zoezi la kuhonga wana Ngara ama la wana Ngara kupuuzia kutundika picha zako majumbani mwao, basi isiwe ni njia ya kuadhibu wasaidizi. Wasaidizi hawajashindwa kazi, ni kwamba wamekupatia heshima kwa kujing’atua kukutumikia. Ni wananchi waliokataa kupokea kile unachojaribu kuwashawishi kwani hakina mantiki katika maisha yao. Wananchi wanategemea maendeleo na sio ahadi zisizosindikizwa na matunda yanayotokana na uongozi wako.
Pia kutofautiana mawazo na mtu kusizae uhasama. Tumia muda mwingi kuongeza idadi ya marafiki na sio maadui. Anayekupenda ni yule anayekwambia ukweli na sio kile unachotaka kusikia. Ogopa yule ambaye anajipendekeza kwa kuwambia yale unayotaka kusikia na adui wa kweli hatoonyesha utofauti wenu hadharani. Kwa hiyo, awe ni mfanyakazi ama mtu yoyote tuu kwako, anahaki ya kukataa ama kupokea kile anachoambiwa. Ni haki ya kila mtanzania kubadilisha kazi na kuegemea busara anapoona mambo yapoenda siko.