




Na Juventus Juvenary
Wawakilishi wa Kata mbalimbali za Wilaya ya Ngara (Madiwani wa Umoja) wamekutana Jijini Dar es Salaam kupitia Umoja wa Wana Ngara kwa lengo la kujadili mshikamano, ushirikiano na maendeleo ya wanachama wao.
Kikao hicho kilifanyika Mei 02, 2026 katika Ukumbi wa Laizer Royal Hotel uliopo eneo la Sinza, ambapo wajumbe walijadili na kuweka kanuni zitakazoongoza Umoja huo ili kuimarisha mahusiano na maendeleo ya wana Ngara waliopo ndani na nje ya Wilaya hiyo.
Umoja wa Wana Ngara umekuwa hufanya vikao vya mara kwa mara kila mwaka kwa lengo la kujadili maendeleo ya wanachama, kusaidiana katika changamoto mbalimbali pamoja na kupanga mikakati ya maendeleo kwa manufaa ya jamii ya wana Ngara.
