Kauli ya Mwenyekiti UVCCM Kagera Kupoteza Watu Ni Kinga

By admin Apr 19, 2024

… Mheshimiwa Rais Samia njoo Kagera utuondolee huu uchafu.

Kupitia mikutano yake katika wilaya ya Ngara, Mwenyekiti wa umoja wa Vijana CCM Mkoa wa kagera Faris Buruhan alisikika akitoa maagizo kwa Jeshi la Polisi kuwa wananchi watakaopotezwa wasitafute.

Kauli hiyo ni ya kijinga,inatakiwa kulaaniwa na kila mtanzania mwenye akili timamu bila kujali itikadi,Dini wala kabila.

Kitendo cha kutoa kauli za kijinga namna hiyo mbele ya Viongozi wa Chama kupitia kamati ya utekelezaji mkoa,Viongozi wa Chama wilaya ya Ngara,Usalama na Wilaya kwa ujumla ni udhalilishaji wa hali yajuu.

Licha ya tamko la katibu mkuu wa CCM Taifa Emanuel Nchimbi kulaani kauli ya Kijana wa UVCCM Faris Buruhani,binafsi ningetamani sana kuona tamko la Uongozi wa CCM wilaya ya Ngara.

Tamko la Wilaya linaweza kutuondoa katika hali tunayoishuhudia kunyukana kusikoisha na kukipaka matope Chama.

“Kama kuna mtu  andhani anao uhuru wa kukaa mttamdanoni kutwa nzimana kisimu chake anashinda mtandaoni anatukana viongozi, Jeshi la Polisi hawa tukiwapoteza msiwatafute! Piga makofi kwa CCM” kauli ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa kagera Faris Buruhani.

Kauli hiyo imelaaniwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dkt. Emanuel Nchimbi aliyenukiliwa akisema  “na leo akiinuka kijana wa CCM kwa mfano akasema wapinzani wetu wakifanya hivi na hivi lazoima tuwapoteze huyu ni kijana wetu ila kasema jambo la kijinga lazima tutalipinga na lazima tuone ni la kijinga kwasababu mwisho wa siku nchi hii ni yetu sote”.

Nitumie kona hii kumuomba mheshimiwa Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi CCM Taifa Dkt samia Suluhu Hassan katika Mipango yake afanya ziara kuja Kagera hasa Wilayani Ngara kuzungumza na Chama,kamati zake ili kuondoa huu Uchafu unaosababishwa na Vijana wajinga wapenda sifa na wanaofanya kila aina ya maovu kutafuta Uongozi.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *