Kundi la maprofesa waliitwa kupanda ndege.
Milango ilipofungwa maprofesa wote walifahamishwa kuwa ndege hiyo imetengenezwa na wanafunzi wao.
Maprofesa wote wakakimbilia kwenye mlango wa ndege wakiomba kushuka.
Isipokuwa profesa mmoja tu alibaki ameketi kwa ujasiri na utulivu.
Kuna mtu alimuuliza, “kwanini hauhangaiki kushuka kwenye ndege kama wenzako?”
Profesa akajibu kwa kujiamini,
“Ni wanafunzi wangu waliunda hii ndege”.
Akaulizwa tena, “Kwahiyo una uhakika uliwafundisha vizuri? Profesa alijibu;
“Kama ni wanafunzi wangu, Nina uhakika haitopaa.”