VIJANA WA NGARA MNAVUNA MLICHOPANDA AU MNAJIFUNZA KUPANDA MTAKACHOVUNA?

By admin Mar 11, 2024
Ambaye yupo tayari kutumika kama daraja la mambo mema achukue na aongoze jimbo. Hamna mtu mwenye hati miliki na hii sehemu, ila yule ambaye yupo tayari kuleta maendeleo yanayoonekana kwa macho na si porojo tulizozowea, basi Ngara ipo wapi na wanangara tutaku support. Tunataka viongozi na sio vielelezo vinavyojiita wahemiwa. Uheshimiwa pembeni, tia usomi , dharau, na ujigambo pembeni na tengeneza maendeleo na si simulizi na vitisho vilivyozoweleka. Kiu chetu ni Kupata Ngara Yenye Nuru.

Kijana, angalia hali yako ya maisha, unapenda unapoishi leo, ama ungependa siku zirudi nyuma ili uishi maisha uliyoishi miaka minne iliyopita. Hivi unaweza kuvuta picha ya maisha utakayoishi miaka mitatu, ama sita ijayo kutoka leo? Utaishi maisha mazuri ama hutokua na progress na utataka uishi maisha unayoishi leo? Pengine leo unapuyanga na kutumika kama chawa na hujui unayemtukuza leo kama hatokuwepo hapo alipo miaka kadhaa mbele. Any ways, fikiri, tadhimini na anza kujiandaa na hali yako ya kesho. Leo unaweza kuwa umepewa pesa uoe ila baada ya ndoa itabidi utafute chakula cha kumlisha huyo uliyeolewa/owa ama zaa ama zalisha. Huo utakua msalaba wako, plan for tomorrow, tomorrow is a secrete as no one knows about tomorrow.

Anyways, nazikumbuka mbwembwe na mbambamba kibao miezi ya mwanzo wa Utawala wa Mbunge mliyempa Sifa za kukaribia Yesu!!!!

Mkamvimbisha kichwa kwa Sifa kibao!!!! Majina mengi ya kumtukuza na kufikia hatua ya kuwadharau na kudhalilisha watangulizi wake,jamani!!!!

Mkamuimbia nyimbo za Sifa na utukufu wa mi5 tena.

Vijana, jifunzeni jambo Kupitia Ubunge. Ndio maana wananchi wapo kimya wakisubiri uchaguzi ufike.

Ni uchaguzi utakaotoa hukumu ya kuwalipa makosa mliyofanya, kifuta majeraha waliyonayo, wasanii waliochapwa viboko, kuteswa na kuachwa na makovu ambayo leo yanawakilisha uongozi wa kijana mwenzenu. Ama kuna msanii alizolea maumvu kwa amri ya mheshimiwa kipindi wale baba, na babu zetu wanaongoza jimbo, kipindi tulikua tunavuka bara bara kwenda shule bila kuhofia magari yanayosafiri mbio na king’ora kana kwamba ni dhahabu zinawahishwa bank.

But all in all, wale walioumizwa, muda ukifika mtafutwa machozi. Najua mpo wengi ila mnaogopa kujitokeza. Nawaelewa kuendelea kujificha chini ya daraja mpaka mvua iishe. Ipo siku hutoogopa na kuwa mkakamavu kwani hutoyayuka hata mvua ikikudondokea. Hawa wanaosifia sifia watakodolewa macho na kujifanya waliimba na kujipendekeza ili maisha yasogee ila ukweli utabaki pale pale, maisha yalisogea bila kuwaacha na makovu ambayo wananchi wengi wameyafunika na mioyo yao tuu. Wapo kimya ili wasiivamie amani na ipo siku watafunguka na bado amani haitovurugika. It is a matter of time, tuu.

Kuna walioamini wamefika, na kabla safari haijafika mwisho wakateremshwa njiani wengine wakiwemo ndugu wa damu!

Wapo waliopachikwa majina mabaya, kufukuza kazi, kuchonganishwa Serikalini, kutishwa na hata kufanyiwa majaribio ya Vifo!

Kila mmoja kwa nafasi yake aombe haki itendeke na kupatiwa anachostahili, si kwa dharau hizo.

Udanganyifu umekuwa mbinu ya kutawala. Kila aina ya fanikio Kimaendeleo umeleta wewe, eeh?? Aibuu kwamba watangulizi wako hawakufanya kitu? Leo kwenye mikutano yako jipachike na kujinadi kwa vitu vilipandikizwa na waliokutangulia ila leo kwa kuwa ndio tunavuna, basi jinyakulie sifa.

Muda mwingine ukijtamba unasikika kama vile Serikali haikufanya? Chama tawala je, na chenyewe ulifanikiwa kuzidi akili za wale waliowekwa ukawakuta wamesinzia na uliwasiri tuu wakaamka na kuanza kuchapa kazi. Kama nakosea, samahani ila kwa leo acha tuu ni seme, Dogo acha dharau.

Na kabla sijaweka peni chini, ni wazi kuwa kwenye majimbo mengine ya Wabunge wanaojitambua wanafurahia maendeleo ya wananchi na sio upimbi wa kubambikizia kesi wafanyabiashara unaoendelea na kugeuzwa kuwa fasheni hapa kwetu.

Sio kuchukia wenye maono na matamanio ya mafanikio na kuwaita maadui. Wapende hata kama wakuzidi busara na utundu wa kuleta miradi inayoweza kuleta manufaa kwa wengi. Sio ukomalie miradi ambayo na wewe ni lazima ujipenyeze na uwe mmoja wa mleta mradi kama ule wa kiwanda cha pombe na biashara kadhaa ulizonazo.

Si kila mwenye mwanufa anataka Ubunge. Hata akiutaka huna mamlaka ya kuzuia watu kuongoza, kwani wewe ulizaliwa na Ubunge?

Eti Kuna watu wanajiandaa kuchukua Ubunge wangu? Weka hata BILIONI 10 za zuluma na utapeli zitapigwa.

Ungekuwa ni kiongozi wa maana, ungetusaidia kutokomeza huu Unyanyasaji wa watendaji na maaskari.

Angalia beria zinavyochelewesha safari za Wananchi, na upatikanaji wa huduma nyingine.

Hamasisha Serikali kufungua njia za kibiashara kwa Wananchi, mikopo ipatikane. Sasa kamuda kako kameshayoyoma na hatujui kama utatumia hii kama gia ya kuomba kura ili ulekebishe kile kilichoshindikana miaka minne iliyopita.

Umefika muda ambapo Wana Ngara tuogope kurudi kwetu kisa Pimbi mmoja eti ana kundi la Wahaini wanaoita raia wema Wasaka Ubunge?

Kiu Cha Wana Ngara ni Kupata Ngara Yenye Nuru. Wale wanaoweza kuvusha Wilaya ya Ngara kutoka kwenye huu umasikini anakaribishwa kuwa daraja na kutuvusha hadi ng’ambo. Kiongozi bora ni kiunganishi na mshawishi gundi ya jamii.

Ndugu zangu, kila mwenye Nia njema na Ngara muda umefika wa kuungana na kuisaidia Ngara yetu.

Binafsi tayari nimefika, na itapendeza kama tutaungana, na hata wastaafu karibuni, wale Wanamuziki walioswekwa ndani njooni.

Kuna waliowahi kuwa washirika wake naambiwa hata mtaani hawaonekani, jitokezeni. 

Hodi Ngara. Nipo hapa kwenye ziara, ngoja tuijenge Ngara yenye neema, Ngara yenye nuru kwa kila mtu, awe amekupigia kura ama lah. Vijana tuwe daraja la mambo mema ili baadaye tuvune matunda ambayo yatawakilisha utu wetu kwani hizi siasa zinapita tuu. Kuna maisha baada ya siasa.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *