TAMAA YA UKUU YAMPONZA NA KUMUUMBUA MBUNGE WA JIMBO LA NGARA NDUGU NDAISABA GEORGE RUHORO
Imekuwa ni desturi ya kila mtanzania kwa muda mrefu kutii na kuheshimu madaraka, tamaduni, sera, mipango, sheria *na* miongozo ya nchi yetu pasipokuvunja ustaarabu huo ili kuifanya nchi yetu itawalike.
Kutokana na utovu wa nidhamu, uchu wa madaraka pamoja na tamaa za kuufikia ukuu baadhi ya vijana chipukizi wa uongozi katika taifa hili wamekuwa wakija na mitindo (styles) tofauti tofauti ili kuweza kuusogelea ukuu hali wanajua nidhamu, subira na uwajibikaji ndivyo vitu pekee vinavyoweza kuamua kesho yako iliyobora katika eneo lolote na nafasi yoyote uliyopo.
*MBUNGE wa jimbo la Ngara* ndugu NDAISABA GEORGE RUHORO tangu kuchaguliwa kwake katika nafasi yake amekuwa ni mmoja kati ya watu ambao hawana subira na wenye tamaa na lengo la kuufikia ukuu katika nchi hii. Tabia yake hii imekuwa ikiibua maswali yasiyo na majibu kiasi kwamba imefikia hatua kila mwenye fikra sahihi anamuona mtu wa hovyo anayepuyanga kwa kila kioja anachofanya.
Mugata: Mhamiaji ambaye analalamika kukumbushwa mara kwa mara kuwa yeye si mzaliwa; leo amegeuka kuwa dalali wa uchifu ili asambalatishe mira na desituri za wale wanaoshindwa kumpokea kama mwana Ngara kamili.
ITOSHE KUSEMA KWAMBA *alaumiwe mshauri wake (mratibu wake wa mambo)*.
Tamaa ya ukuu ya ndugu RUHORO katika uongozi wake imekuwa ikijitanabaisha katika mazingira mbalimbali:-
1. Mheshimiwa huyu alianza na tamaa ya kulazimisha kupendwa. Alianzisha program ya kuchapisha na kusambaza picha, mabango na kalenda na kuwasihi watu mbalimbali wanunue, zoezi ambalo kimsingi halikuwa na mapokeo mazuri na mwisho wake likafifia, program ikawa closed.
2. Alivyoona haitoshi, Mheshimiwa huyu akaamua kuanza kuiga styles za kusikiliza wananchi kama alivyokuwa anafanya aliyekuwa katibu wa sera na uenezi CCM taifa Mr. Paul Christian Makonda, utaratibu huo ulimudu kwa muda kidogo ambao kimsingi ulikuwa unaboa hata kwa watumishi wa halmashauri ya Ngara aliokuwa anaambatana nao lengo likiwa waweze kuwajibu wananchi (Makonda style).
3. Haikutosha, Sasa ameona avunje miiko ya mila na desturi za wanangara na kutaka asimikwe kama Chifu kuiga style ya Mheshimiwa Rais wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan aliyesimikwa kuwa CHIEF HANGAYA eneo la Bujora – Mwanza yalipo makubusho ya machifu. *Ikumbukwe kuwa* Lengo la Mheshimiwa Rais kusimikwa hiyo 13 June 2023 ilikuwa ni kupata nguvu ya kimaamuzi kwa machifu wote nchini yaani kama Mkuu wa machifu wote nchini. Sasa haijajulikana ipi ni adhima ya Mbunge wa Jimbo la ngara.
*NI WAZI KWAMBA* ilani za vyama vyote vya siasa hapa nchi haziruhusu kuingilia mila na desturi walizojiwekea watanzania enzi na enzi (mababu na mababu) kwakuwa suala la uchifu ni la koo. Mheshimiwa Mbunge huyu angepaswa kutambua adhima ya Rais kuapishwa kwake kabla hajaanza kuipa nguvu tamaa yake ya huo ukuu.
*NI KWELI* ameahidi kuilea familia ya Chifu balamba endapo itamsimika kuwa Chifu baada ya kuwa imekataa ombi hilo, lakini imani ya wengi ni kwamba familia za Chifu baramba zinajitosheleza kiuchumi kiasi cha kutotaka hisani ya vitu vidogo vidogo.
*Ndugu NDAISABA* anapaswa kutambua kuwa, damu yake haina asili ya kichifu na hivyo haitotokea yeye awe chifu hadi mwisho wa dunia maana ndo desturi za kiafrika zilivyo.
*Kwakuhitimisha*, kama Mbunge ndaisaba anaheshimu mila na desturi za wanangara, anatii miiko ya kichifu na kuheshimu imani za watu na jamii zao, anaheshimu amali za jamii na historia ya kitaifa na utaifa, ameapa kuwa Mbunge na kuulinda katiba na sheria za nchi hii *BASI* ajiepusha maramoja na tamaa za kutafuta ukuu kwa nguvu, hili litamharibia na kumpotezea mvuto siyo tu kwa wanangara bali hata kwa wale wote waliokuwa wanamheshimu ndani na nje ya taifa hili.
*Jamii imetulea, jamii imetukuza, jamii itatuzika – tusichokoze asili tusije tukalaaniwa!*
Mungu ibariki ngara.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ibariki Afrika.