Ngara: Vyombo Vya Usalama, Usalama Udumishwe

By admin Jun 3, 2024
Uchifu: Ulezi wa koo za kichifu si hitaji linalohitajika Wilayani Ngara kwani koo za kichifu zilizopo zinajitosheleza na hazijaomba ulezi kutoka kwa mtu yoyote.

VYOMBO VYA USALAMA NGARA SIMAMIENI KIDETE MATUMIZI SAHIHI YA KIMTANDAO: WAWAJIBISHENI WANAOVUNJA SHERIA ILI KULINDA HADHI YA WATAWALA WETU NA JAMII YA NGARA KWA UJUMLA

Na: Titho Philemon

NIANZE KWA KUSEMA KUWA kwa mujibu wa Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao (The Cybercrimes Act) No. 14 ya Mwaka 2015, ni kosa kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni. Adhabu yake ni faini isiyopungua Shilingi Milion 5 (Tsh 5,000,000/=) au kutumikia jela kifungo kisichopungua Miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

Kwa utangulizi huo, ni wajibu wa kila mtumiaji wa Kimtandao* kuhakikisha anachapisha taarifa ambazo ana uhakika nazo ili kujiepusha kudondokea kwenye mkono wa sheria na hivyo kuifanya sheria ichukue mkondo wake.

Kumekuwa na usambaaji wa makala yenye kichwa:-  ” KAMA MAANDIKO YA JOSIAS CHARLES NDO YALITUMIKA KUITISHA KIKAO CHA WAZEE NI ANGUKO KWA WALIOTENGENEZA PROPAGANDA YA UCHIFU. ” iliyojaa taarifa za uongo, na za uzushi *lengo likiwa* ni kumchonganisha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara (DC) Col. Mathias Julius Kahabi na mamlaka zilizoko juu yake katika nchi hii.

*IKUMBUKWE KUWA* nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Ngara imeanzishwa chini ya *Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Tawala za Mikoa (The Regional Administration Act) No. 19 ya Mwaka 1997 Sura ya 97 Toleo la Mwaka 2019)* na hivyo kumfanya *Col. Mathias Julius Kahabi* atekeleze majukumu yake yote ya kisheria kama anavyoagizwa na sheria hiyo. Pamoja na Mambo mengine Mkuu wa wilaya ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ndani ya wilaya yake ya kiutawala na hivyo kumfanya awe mwenye wajibu wa kukemea, kuonya, kuzuia na kuadhibu matendo yote yenye kuvunja na yenye dalili za kuzorotesha hali ya kiusalama ndani ya wilaya yake ya kiutawala.

Kwa kuwa Mkuu wa Wilaya ndiye msimamizi mkuu wa kiusalama ndani ya wilaya hivyo basi hazuiliwi kwa namna yoyote kukutana na mtu yoyote ndani wilaya yake kwakuwa raia wema (watoa taarifa), walalamikaji, watuhumiwa wa uharifu na wazee washauri (jamii) *wote ni wateja wake kiutawala.

BAADA YA UTANGULIZI HUO MFUPI ninaomba sasa nijielekeze katika kujibu na kuichambua makala ya ndugu JOSIAS CHARLES kijana mwenzangu wa Ngara kama ifuatavyo

Hoja ya UCHIFU ilishafikia tamati kama sehemu ya maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe. Col. Mathias Julius Kahabi kwenye kikao chake kilichomkutanisha na wazee wa Ngara pamoja na viongozi mbalimbali cha Tarehe 28/05/2024 ambapo pamoja na mambo mengine Mheshimiwa DC aliomba jamii iweze kuepukana na tabia hizo na hivyo kuelekeza nguvu zao katika mambo yenye kutuletea maendeleo.

Kitendo cha kijana mwenzangu JOSIAS CHARLES kuendelea kukosoa uamuzi huo ni kutaka kudhihirisha kuwa hajaridhishwa na kile kilichoamriwa. Kwa maana hiyo ninamshauri aende kokote kule atakapohisi anaweza akapatiwa msaada katika mamlaka zilizopo juu ya DC kwa kile anachohisi kitakuwa jawabu sahihi na litakalomridhisha. Wanangara tutasimama na DC wetu.

Kuhusu hoja ya Mhe. Mbunge kuombwa kulea koo za Ngara ukweli ni kwamba ukoo wake pekee (Abatasha) ndo uliomuomba awe mlezi kwakuwa na yeye ni sehemu ya ukoo huo lakini kilichokuja kustaajabisha ni kuona ushawishi unaongezeka kwa koo zingine yeye (Mbunge) kuziomba azilee pia ikiwa ni pamoja na koo za kichifu (Chief BALAMBA na Chief Nsoro) ambapo upande wa CHIEF BALAMBA ulikataa ndipo mwakilishi mmoja wa familia hiyo ya kichifu (Pius BALAMBA) Tarehe 07/05/2024 alipoandika makala ya kuchukizwa na maombi hayo na hivyo kuweka msimamo wa kutoliunga mkono suala hilo wao kama familia ya kichifu huku wakiamini kuwa kwa asili chifu hutokana na familia ya kichifu kwa uteuzi wa kurithishana na siyo ulezi wa damu ya nje ya familia husika.

Katika hili la uchifu ninaomba nitafakari na JOSIAS CHARLES pamoja na wanangara katika hoja zifuatazo:

1. Kama ukoo wake wa Abatasha ndio uliomuomba aulee (Jambo la kheri kabisa) kama mmoja wa ukoo huo, ni kipi kilimfanya aanze kufikiria kuzilea koo zingine zikiwemo na za kichifu wakati anajua yeye siyo wa damu ile kama ilivyo desturi ?

2. Press Conference ya kupinga Mbunge kupewa uchifu ya Tarehe 10/05/2024 ikihusisha wazee maarufu wa Ngara na wawakilishi wa Familia za Kichifu iliwaibua wazee, huku wakikemea kwa uzito na msisitizo mkubwa tamaa ya kijana wao kutaka kutawazwa kuwa chifu. Je JOSIAS CHARLES unajua tukio lililofuata usiku baada ya press hiyo ?

Baada ya kumalizika na kupandishwa hewani kwa Press ya wazee wa Ngara kupinga uchifu ya Ijumaa Tarehe 10/05/2024 *jioni hiyo hiyo* katibu wa CCM kata ya Keza *Bwana Paulo Siti* alipigiwa simu na management ya Mbunge kuhusu kuahirishwa kwa zoezi la Jumapili Tarehe 12/05/2024 ambalo lilipaswa kufanyika *Rukira Shule ya Msingi* na hivyo akasambaza taarifa kwa wazee wote wa ukanda wa Bushubi ambao walikuwa wamearikwa kuhudhuria tukio hilo. 

Mambo ya kutafakari hapa ni:

1. Ni Jambo gani liliahirishwa hiyo Ijumaa ya tarehe 10/05/2024 ambalo lingefanyikia pale Rukira Primary School ?

2. Kama jambo hilo lilikuwa jema kwanini liahirishwe kwa kushtukiza kiasi hicho yaani siku moja na masaa kadhaa kabla ya tukio ?

3. Kwanini tukio hilo la Rukia Shule ya Msingi liahirishwe mara baada ya Press Conference ya wazee iliyokuwa inapinga uchifu ?

4. Kwanini tukio hilo lihusishe wazee na wazee ndo wapewe mwaliko ?

5. Lilikuwa ni tukio gani ?

Kijana mwenzangu JOSIAS CHARLES kwa mujibu wa Kifungu cha 16(2) cha Sheria ya Tawala za Mikoa (The Regional Administration Act) No. 19 ya Mwaka 1997 Sura ya 97 Toleo la Mwaka 2019 Mkuu wa Wilaya anamshauri wake kiutendaji ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya (The District Administrative Secretary – DAS) ambao kwa umoja wao hutafakari michakato ya kiusalama, kimaendeleo na ustawi wa jamii na hatimaye kutupatia mikakati yaknifu yenye kubadirisha taswira mbovu na kujenga taswira njema katika wilaya yetu. Je unataka kila wanaokutana na DC ofisini kwake ujue walienda kuongea naye nini ? Unataka ujue wewe kama nani ? Wewe ni afisa habari wa halmashauri ? Who are you by the way Kaka?

*Kwa maana hiyo*, uchambuzi wako katika tukio lako la Tano ni uchambuzi ambao kimsingi hauna nguvu kiutawala na haueleweki (unreasonable). 

NI DHAHIRI SASA KUWA kitendo cha Tarehe 28/05/2024 cha Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe. Col. Mathias Julius kukutana na wazee wa koo za Ngara Ngara eneo la wazi, kwenye haraiki mbele ya kamati yake ya ulinzi na usalama ya wilaya na mbele ya waandishi na vyombo vya habari kimefungua ukrasa mpya wa mshikamano wa kisiasa na kijamii ndani ya Ngara, hivyo basi ni jukumu la wanajamii wote wa Ngara kulinda tunu ya usalama na amani ambayo ilisisitizwa na mkuu wa wilaya katika kikao chake hicho cha Mei 28, 2024 kama sehemu ya kujenga taifa imara na jamii isiyo na mipasuko. 

Vyombo vya Dola vinalo jukumu sasa la kuhakikisha linawatia nguvuni yeyote atakayejaribu au kuamua kuzua taharuki upya ya kiusalama kwa wazee wetu, watawala wetu na jamii nzima kwa ujumla. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeimarisha misingi bora ya kiusalama ndani ya Ngara itakayodumu kwa kipindi kirefu na hivyo kutengeneza vizazi sahihi na shupavu ambavyo pia vitakuwa fahari ya Tanzania kwa hali ya sasa na hapo baadae.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *