Mama Samia, Mkimaliza kwa Makonda, Mje Ngara kwa Mbunge

By admin Apr 22, 2024
Ngara: Na huku pia Maadili yahitajika

Nimeona link kwa Gazeti la Mwananchi kuhusu Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuitwa kwenye Kamati ya maadili.

https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/makonda-aitwa-kamati-ya-maadili-ccm-4598978

Maswali ya Wananchi wengi ni kuhusu Kauli za Bwana Makonda anazotoa na kutafsriliwa kama udhalilishaji kwa Viongozi na watendaji wa Serikali.

Ikiwa hihizo Kauli zimepelekea kuitwa kuhijiwa, basi mkimaliza mje na Ngara, au mumuite huyu Mbunge.

Mara nyingi kwenye mikutano yake amekuwa na kawaida ya kudhalilisha watu hasa wastaafu wenye nguvu akiamini ndio washindani wake Kisiasa.

Anafika mbali kwa kuwaita majina ya ajabu na udhalilishaji Kupita kiasi.

Ameweka makundi ya watu kutafuta visa kwa kisingizio cha wanaomsema vibaya na hata kutishia uhai wa watu.

Mheshimiwa mwenyekiti wa Chama Taifa, mama yetu Samia Suluhu ikikupendeza zipe Mamlaka Kamati za maadili zianze kufanyia kazi Wabunge wenye karba ya Ndaisaba maana wanakidhalilisha Chama.

Kamati ya maadili yamuita Makonda

Juzi, aliskika Katibu mkuu wa CCM Taifa Dkt. Emanuel Nchimbi akikemea tabia za baadhi ya Wana CCM wenye uchu wa madaraka.

Nikuhakikishie , kama Kuna mtu mwenye uchu wa madaraka ni huyu Mbunge ambaye ana makundi ya watu waliojitayarisha kumrudisha madarakani kwa gharama zozote.

Tunaamini CCM ni Chama Cha Wananchi wote,SI cha wateule fulani. Tusaidie

Nakutakia kazi njema, na Ziara njema yenye mafanikio kwa Watanzania. Mungu akubariki.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *